Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Kituo cha Daladala Simu2000 kimefungwa leo Septemba 14, 2024 kupisha ujenzi wa karakana ya mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi.
Karakana hiyo ni kwa ajili ya mradi wa mabasi hayo awamu ya nne. Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia Mkuu wa Idara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Mary Mwakyosi akizungumza na Mwananchi ameeleza hayo.
Hata hivyo, Julai 13 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alifanya mkutano na wafanyabiashara hao akawaeleza manufaa ya mradi huo, akiwaahidi watatengenezewa mazingira mazuri ya kuendelea na biashara zao wakati wa ujenzi wa mradi huo.
Awamu ya nne ya mradi huo inahusisha mabasi yatakayotoka Tegeta, Mwenge hadi Ubungo kupitia Barabara ya Sam Nujoma. Karakana hiyo inatarajiwa kukamilika ujenzi wake Machi, 2025.
Katika eneo hilo, Mwananchi imeshuhudia maandalizi ya kuifunga stendi hiyo yakiendelea. Jirani na mageti ya kuingia na kutokea daladala kumewekwa utepe mwekundu na muda mupi baada mabasi yakazuiwa kuingia ndani.