Stendi ya Mizigo Bariadi ya Bilioni moja, inakusanya Sh. 0 Mwezi mzima

Stendi ya Mizigo Bariadi ya Bilioni moja, inakusanya Sh. 0 Mwezi mzima

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
vlcsnap-2023-09-01-00h31m20s102.png


Kuna vitu huwa vinachekesha sana kwenye hii nchi yetu, unafikiria kweli tunao watalaamu wa kutosha? Wanaoweza kung’amua mambo na yakawa sawa? Yakaleta tija kwa taifa?

Angalieni hiki kituko, uko katika Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ndani ya Mkoa wa Simiyu.

Halmashauri hiyo ilijenga stendi ya Mizigo eneo la Kidulya takribani kilometa 7 kutoka mjini Katikati, ambayo iligharimu zaidi ya Sh. Bilioni moja.

Mshangao mkubwa hapa, Stendi hiyo licha ya kugharimu kiasi kikubwa cha pesa, lakini kimekuwa chanzo nfu cha mapato kwenye halmashauri hiyo.

Taarifa za ndani zimeomyesha kuwa, ndani ya mwezi mzima Stendi hiyo imekusanya mapato Sh. 0 (yaani hakuna mapato yeyote yaliyokusanywa kwa mwezi mzima)

Unajua hii inastahajabisha, stendi ya Bilioni 1 tena na zaidi, alafu mwezi mzima hakuna mapato yamekusanywa, unajiuliza Nani? Alibuni huu mradi, Ni kweli Serikali ina pesa za kuchezea?

Nimefuatilia kujua sababu ni Nini? Moja ni kwamba wafanyabiashara wamegoma kushushia mizigo yao kwenye hiyo stendi kutokana na umbali.

Pili stendi hiyo haina miundombinu ya kuwezesha usalama wa bidhaa za wafanyabiashara kuwa salama hasa nyakati za mvua.

Tatu stendi hiyo haina kivuli kwa ajili ya kujikinga mvua au jua kwa wafanyabishara, na wala haina stoo ya kuhifadhi bidhaa pamoja na kukosa ulinzi wa kutosha.

Wafanyabiashara wanasema, umbali wa Kilometa 7 kufika kwenye hiyo stendi kutoka mjini, ndiyo kikwazo kikubwa, wakishushia uko mizigo inawaongezea gharama kubwa kufikisha mizigo mjini.

Mfano nikishushia mizigo kule stendi, alafu nikachukua gari ndigo (Canter) ghamara yake kuleta mzingi hapa mjini katikatika siyo chini ya 300,000, faida yote inasha, lakini kule hakuna stoo ya kuhifadhi mizingo, sasa mvua ikinyesha tutaweka wapi mizigo yetu?

Kutokana na hali hiyo, stendi hiyo ufikia wakati mwezi mzima hakuna gari lolote ambalo limeingia kushusha mzingo, hivyo makusanyo ni Sh. 0 kwa mwezi, na yakiingia hayawezi kuzidi mawili tu, hapo utahesabu mapato haya yakipatikana inawezekana kwa mwezi ikakusanya kidogo sana.

Wafanyabisha wamesusia hiyo stendi, na walichokifanya ni kutafuta eneo ambalo lipo uchochoroni, mtaa wa Butiama na kufanya kuwa stendi bubu ya mizigo, wao wanasema eneo hilo lipo karibu sana na mjini.

Unajiuliza Nani? Alibuni huo mradi kupelekwa uko? Je hatuoni kuwa aliingizia hasara serikali? Eneo rafiki lilikosekana mjini? Kwa nini eneo la Mnada usingehamishwa mnada na kujengwa hiyo stendi?

Stendi kukusanya Sh. 0 kwa Mwezi mzima, alafu iligharimu zaidi ya Bilioni moja ni hasara kubwa sana.
 
Na hapo ukute aliye plan hii kitu yuko ofisini, na soon anakuna na mpango mwingine kama huu

Na analipwa mshahara mkubwa
Na semina za kutosha kila week

Na marupu rupu kibao analipwa
 
Ni Afadhali kujenga ikaonekana kuliko kuibwa ikiwa kwenye papers.

Matunda utayaona mbeleni.
 
Na hapo ukute aliye plan hii kitu yuko ofisini, na soon anakuna na mpango mwingine kama huu

Na analipwa mshahara mkubwa
Na semina za kutosha kila week

Na marupu rupu kibao analipwa
Na hata akichukuliwa hatua, iankuwa ni kuhamishwa kituo cha kazi !!!
 
Bahati nzuri bariadi napafahamu na hiyo stand naifahamu. Ilijengwa wakati wa RC Mtaka, pia ofisi kadhaa zimewekwa maeneo hayo mf TANROAD.

1. Kuiweka hapo ilikuwa ni sawa kabisa kwani magari makubwa ya mizigo kuingia mjini sio sawa kabisa. Pia unatoa ajira kwa gari ndogo za mizigo, mama lishe, unatanua mji n.k

2. Km 7 nenda rudi ni km 14, lita 4 ambazo ni sawa na sh 15,000/-. Ukikodi guta la mizigo haizidi ef 50.

3. Hivyo visingizio vingine havina mashiko. Ulinzi si polisi wawili tu au sumajkt wanawekwa. Kivuli banda si linawekwa?

kilichopo hapo hakuna utashi, na shida halmashauri inacollude na wafanyabiashara.
 
Na hapo ukute aliye plan hii kitu yuko ofisini, na soon anakuna na mpango mwingine kama huu

Na analipwa mshahara mkubwa
Na semina za kutosha kila week

Na marupu rupu kibao analipwa
Mzee, huwezi plan Stand ya mizigo bila consultation na jumuiya ya wafanyabiashara wa eneo husika. Tatizo siku zote Mfanyabiashara hataki cost mpya kwenye biashara, shida hapo mkurugenzi atakuwa anazuiwa na ccm bariadi kutekeleza uhamaji.
 
Utaambiwa tunapanua mji , akili mbovu Sana hzi ...!! Majitu yaliyokaa ofsini huwa hayajui chochote , na yanafanya mipango bila kuhusisha watu wa usafrishaji yanachofkria yenyewe yanaona ni Sawa mwisho inakuwa total loss , mpak matunda yaje kuonekana ni miaka nenda Rudi ....
 
Kama truck ina mzigo wa tani 30 unahitaji center ngapi kwa gharama ya 50k kwa trip?. nadhani itakuwa zaidi ya 10.sasa faida itakuwepo kweli?
 
Back
Top Bottom