KERO Stendi ya Nane Nane Mbeya gizani kwa kukosa Luku, viongozi washtumiwa kwa kutowajibika

KERO Stendi ya Nane Nane Mbeya gizani kwa kukosa Luku, viongozi washtumiwa kwa kutowajibika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ni jambo la kusikitisha kuona stendi ya Nane Nane, Mbeya, ambayo ni kitovu cha usafiri kwa abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini, ikiwa gizani.
IMG_2147.jpeg

Stendi hii ni chanzo kikubwa cha mapato kwa serikali kupitia kodi na ushuru unaolipwa na wajasiriamali na abiria kupitia tiketi, hivyo inapaswa kuwa mfano wa utoaji huduma bora kwa umma.
IMG_2147.jpeg

Kukosekana kwa taa katika eneo hili kunahatarisha usalama wa abiria na mali zao, jambo linalosababisha wasiwasi miongoni mwa watumiaji wa stendi. Aidha, hali hii inadhoofisha maendeleo ya huduma za umma na kudhihirisha uzembe wa viongozi katika kusimamia maeneo yenye umuhimu mkubwa kiuchumi na kijamii.

Inasikitisha zaidi kusikia kuwa tatizo hili limetokana na kuisha kwa Luku, na bado viongozi hawajachukua hatua yoyote ya kurejesha huduma ya umeme.

Mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua za haraka kurejesha umeme na kuhakikisha usalama wa stendi hii muhimu. Viongozi wanapaswa kuwajibika ili kuondoa changamoto zinazoweza kudhoofisha ustawi wa abiria na uchumi wa jiji la Mbeya.
IMG_2149.jpeg
 
Back
Top Bottom