Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Maisha yananenda kinyumenyume, watu wamekuwa wakitoa maoni kuwa beat zangu ni nzuri wakati mimi huwa nazifanya nikiwa siziamini kabisa. huku ninakojipinda bado watu hawanielewi. πππMkuu,
Bado sitakuwa mbali Sana na ushauri wangu wa Mara ya mwisho though Kuna kitu Cha tofauti Leo nimekigundua kwako.
Leo nimegundua una sauti ya kufanya voice over,jaribu kujitafuta huko pia.
Kuhusu kurap nasema bado sana, nakuona mwepesi mno,hasa Kama una lengo la kuwa msanii wa mainstream Media.
Kwenye kuntengeneza beat uko vizuri Sana,nakumbuka nilishawahi kukuambia.
Yote kwa yote,Leo naona umeimprove tofauti na Mara ya mwisho.Nyimbo zako zote mbili zinasikilizika ingawa si Sana,maana binafsi siwezi kuweka kwenye repeat mode. Cha kukushauri zaidi ni endelea kukaza kwenye uandishi,bado una uandishi mwepesi mkuu.
Kuna mdau mmoja mkubwa Sana wa burudani hapa bongo ngoja Leo nimsikilizishe hizi nyimbo zote mbili alafu nimsikie maoni yake. Atakachoniambia nitakuja kuandika hapa pia.
Ngoja tusikie maoni ya wengine pia.
Kwa kuwa wewe ni msanii mpya unayechipukia sitakwenda mbali na walio level yako,I mean wasanii wa kisasa ambao wanafanya vizuri.Maisha yananenda kinyumenyume, watu wamekuwa wakitoa maoni kuwa beat zangu ni nzuri wakati mimi huwa nazifanya nikiwa siziamini kabisa. huku ninakojipinda bado watu hawanielewi. πππ
but kama naimprove ni jambo zuri, kuhusu voice over nitalitizama hilo pia.
kwenye uandishi ni nani unamkubali kwa mfano ili pengine nipate darasa huko...
Hapo namba 2 ndo ulimwengu niupendao. Vina namsikiliza sana, hao wengine siyo kivile ila nitaongeza nyimbo zao kwenye playlist nione nasogeaje mbele.Kwa kuwa wewe ni msanii mpya unayechipukia sitakwenda mbali na walio level yako,I mean wasanii wa kisasa ambao wanafanya vizuri.
Na ushauri wangu ni huu;
1.Kama unataka hela,fame na interviews jifunze kwa Rapcha. Ana uandishi uliokomaa na anachana kwa swagger,nyimbo zake zinapendwa na mademu na anaenda na upepo wa soko linavyotaka.
2. Kama unaamini katika misimamo na njia zako bila kujali utapata shows, interviews na pesa (namba ndogo on-line) huku mziki wako ukiwaimbia watu maalum wanaokuelewa na kukusuport basi Kuna Hawa madogo kina kadgo kitengo,dizasta vina maradona na Mex. Ila Hawa kwa uandishi wako inabidi utulize kichwa kwelikweli,ila kwa kuwa unataka kujifunza lolote linawezekana mkuu.
Chaguo ni lako mkuu.
πHujaitendea haki beat, umepoa sana
Unaonekana ni mtu fulani innocent sana