Steps kuelekea ndoa

Hiyo ndo nilishampa kama homework,nasubiria majibu nadhani itakua nzuri zaidi!.
Thanks!
 
bwananyie mnaleta complication za ajabu .kwetu sisi wachaga huwa tunamchukua mwamnamke tunamweka ndania asubuhi mzee anaamka na mbuzi anapeleka kwa wakwe ngomo inaishia hapo unakuwa tayari umeshaoa


kijana uchaga wa kizamani huo.
 
Du!! Mkuu hiyo sidhani kama inawezekana kwangu,Kwani nataka Ndoa ya kanisani!
Ndoa sio kanisani wewee!!.....ina maana unataka kufuata mlolongo wa mila sijui madudu gani ili uende kanisani au ili uingie kwenye ndoa?
 
Du!! Mkuu hiyo sidhani kama inawezekana kwangu,Kwani nataka Ndoa ya kanisani!

Ndoa sio kanisani wewee!!.....ina maana unataka kufuata mlolongo wa mila sijui madudu gani ili uende kanisani au ili uingie kwenye ndoa?

Birigita hiyo pointi muhimu sana. Watu wanasahau ukienda kanisani/msikitini ni mila inayojitegemea na ukiweka ndani mzee apeleke mbuzi nayo ni mila inayojitegema. Unaweza kuchanganya na ndo maana kuna zoezi linitwa kubariki ndoa
 
jamani ndugu zangu kuelekea ndoa ni pagumu sana na sijui sisi kama wanaume tunampango gani maana dada zetu wamekuwa kama pweza wanacheza karata katika ndoa tusaidiane wanaume kwa ushauri me sijaingia katika ndoa ila naona mambo yanavyofanyika kwa wenzangu na mimi pia nia hatari
 
hii mambo imetofautiana toka kabila moja hadi jingine kaka, nway utapata majibu kwa wale wa jamii yako
 
tafuta mshenga
 
kweli mkuu maana lazima ajue kwani kabila zingine wanakuwa kama valey ya baiskel asije akakataliwa au vipi hapo wakuu mmmh
Conquest-kwetu uchumba unakwea mbuyu
 

Kwa uwelewa wangu Ndoa ni mchakato wa kijamii na kisheria, ndio maana mtu akiingia ndani ya Ndoa ana haki fulani fulani za kisheria na kijamii. Ndoa bwana ina mlolongo ufuatao:

1. Uhiari (consent) ya wote wawili bila ya kushawishiwa na mtu wa tatu (third part)
2. Kujitambulisha (declaration) - mkishakubaliana inabidi watu wajue, hapo ndio wengine wanasema pete ya uchumba, labda nenda kwa wazazi, au tuma mshenga n.k.
3. Shukrani (appreciation) - shukrani hii inaweza kuwa katika mfumo wa mahali au malipo fulani au kitendo fulani cha kuonyesha shukrani kwa wale wote waliochangia kwa namna moja au nyingine mpaka nyinyi wawili mkafikia hapo. Yaweza kuwa umezaliwa ukatoa shukrani kwa wazazi au umersomeshwa n.k.
4. Utambulisho kwa Umma (public event) - ndoa ni mchakato wa kijamii, hivyo umma inabidi ujulishwe. Hapa kuna matangazo ya ndoa na kitendo chenyewe cha kwenda aidha kanisani au kwa shekh au kwa chifu na kufungishwa ndoa. Lazima umma ujulishwe ili kuondoa migongano baada ya kufungishwa ndoa. Maana kabla ya hapo any body can pair with you without breaking any law.
5. Ratification (au intimacy relationship) - yaani kitu cha mwisho ambacho kinakamilisha ndoa ni kile kitendo cha wawili hawa kupeana kile mwenzako anakosa (to complimate each other) - bila ya kuzunguka sana watu wengi hukiita "tendo la ndoa".

Bila ya hayo kutimia ndoa hiyo ni "bugulu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…