Stesheni za SGR ambazo zimepewa majina ya viongozi ziwe pia ni sehemu ya kujifunza na kufahamu historia za viongozi hao

Stesheni za SGR ambazo zimepewa majina ya viongozi ziwe pia ni sehemu ya kujifunza na kufahamu historia za viongozi hao

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Kwako Rais wa JMT

Mhe. Samia Suluhu Hassan,

Ninakusalimu kwa jina la JMT,

Kufuatia uzinduzi rasmi wa safari za SGR, Dsm- Dom uliofanya siku ya 01/08/2024 na Taifa kuandika historia ya kipekee katika ukamilikaji wa mradi huo mkubwa ambapo sambamba na uzinduzi wa safari hiyo pia tukio hilo liliambatana na kuviita majina vituo vya stesheni za SGR.

Kulingana na majina ya vituo hivyo ni faraja kubwa vimeitwa kwa majina ya viongozi wetu wastaafu, waasisi na jina lako kufuatia hilo nina maoni katika hili la kuviita majina ya viongozi vituo vya stesheni ya SGR.

Kwa kuwa viongozi hao walilitumikia Taifa hili kwa uzalendo na uadilifu na kwa kuwa tunapenda historia ya uongozi na utumishi wa iendelee kujulikana na kufahamika, ninapendekeza kila kituo cha SGR kilichopewa jina la kiongozi iwe ni kama maktaba maalumu ya kuonesha historia ya kiongozi huyo.

Kwenye kuta za stesheni ziwekwe picha za zenye kuelezea historia ya kiongozi huyo na hata kwenye Televisheni zilizopo humo ioneshwe historia ya kiongozi huyo kwa kuwa Reli itatumiwa na wengi hivyo itakuwa ni njia rahisi kuifundisha historia ya viongozi wetu. Ahsante mama kwa SGR
 
Hilo litasaidiaje kuondowa umasikini katika hivyo vijiji?
 
Back
Top Bottom