KOMEDIANI maarufu na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere' amesema anatarajia kugombea na kushinda ubunge 2015 bila kutumia fedha.
Akitema madini mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, Steve alisema atagombea kupitia Jimbo la Kinondoni, lakini ieleweke kuwa hatotumia fedha katika kampeni zake.
"Saundi (maneno) ndiyo kila kitu, ukiongea na watu vizuri na wakakuelewa, hakuna kitakachoshindikana, nitaibuka na ushindi mzito tu, vuteni subira watu wangu," alisema Nyerere.
Bunge letu limekuwa la hovyo, ni baada ya mtu kama mganga profesa maji marefu kuwa wabunge kwa kutumia ndumba, hasa kuwasindika viongozi!!!!! Sasa kila mtu ana amini anaweza kuwa mbunge!