Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Ni kijana mzaliwa wa mkoa wa Shinyanga, wilaya ya Kishapu, katika kijiji cha Ukenyenge.
Ni msomi kutokea chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Masele ni mmoja wa vijana waliopata bahati ya kuaminika na chama kikongwe cha CCM. Na kwalo alibahatika kushika nyadhifa mbalimbali hadi kufikia ngazi ya Unaibu wa Waziri serikalini.
Wahenga walipata kunena, mgema akisifiwa tembo hulitia maji! Na ndicho kilichotokea kwa kijana huyo pale alipoanza kulewa sifa na kupelekea kuwavimbia kichwa Wakuu wake wa kazi kwa kujikweza na kutaka utukufu wa kuhimidiwa ilhali nyakati hizo hazijawa kwake.
Ile kulazimisha apatiwe ulinzi wa TISS kwa kigezo cha yeye kuwa ni naibu Rais wa Bunge la Afrika, hakika kilimharibia kila lililo tarajiwa kwake!
Ifahamike, mfumo wa uadilifu haupo sehemu ya mjikwezi.
Steven ajilaumu mwenyewe.