TANZIA Steven Msaki bishoo wa Mbezi Beach afariki dunia

Uko sahihi Steve kama Steve hakuwahi kupata shida ndogondogo na ni bahati mbaya tu kuwa kwenye familia yao alichagua aina ya maisha hayo way back 1998 alishajitumbukiza kwenye ulevi,hatumsimangi marehemu ila tunafundishana
 
Uko sahihi Steve kama Steve hakuwahi kupata shida ndogondogo na ni bahati mbaya tu kuwa kwenye familia yao alichagua aina ya maisha hayo way back 1998 alishajitumbukiza kwenye ulevi,hatumsimangi marehemu ila tunafundishana
Upo sahihi
 
Umeongea kikomavu sana
 
AAlcohol free since January 1, 2024.
Ngoja ni share kitu juzi nilipigiwa simu na mama akanambia mwanangu msaidie mdogo wako.

Kifupi mdogo angu ni mtundu toka udogoni na ukituona ni kama mapacha TUMEPISHANA TUMBONI MIEZI SITA..Ina maana ujauzito wake ulitunga Mimi nikiwa na miezi sita.

Kwa Sasa dogo amekua anakunywa Sana na hope Kuna vitu anatumia zaidi ya vilevi vya kawaida maana huwa akilala mpaka aamke mwenyewe. Na tunajua vilevi vina arosto je? Huyu dogo naweza/ tunaweza kutumia mbinu gani aweze kuacha ULEVI? JE? WEWE KAMA WEWE UMEWEZA KWA KUTUMIA MBINU GANI?

Maana Kuna muda unaweza SEMA ngoja u refreshing au kukawa na tafrija au ukatembelea mtu/ watu wanao kunywa ama ukawa na vinywaji changamshi kwenye friji nyumbani je ? unaweza vipi kushinda vishawishi.

min -me
 
Umeongea vyema mkuu
 
Stive amevuta. Apumzike kwa Aman classmate
 
Watu ni tofauti mkuu. Mimi nafikiri nina willpower kubwa nikiamua kitu changu ni lazima nakikamilisha.

Na zaidi najua kutoingia popote kwenye mazingira nisiyoyataka.

Ingawa hata nyumbani nina beer, nina wine, nina Scotch nina Tequila, nina Gin, naziona kila siju, lakini sinywi.
 
Nina kama miaka miwili sijamsikua wala kumuona kabisa. Alikua na changa moto ya kisukari plus unywaji na uvutaji uliopitiliza kuto kulala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…