Stieglers Gorge Hydroelectric Project

GT,

..hata barabara ya kwenda kusini ilikuwa ipitishwe maeneo hayo.

..nilisikia kwamba ilikuwa wajenge bwawa pamoja na daraja.
 
Stiglers Gorge iko Ndani ya Pori la akiba la Selous. Ni sehemu mito mitatu inapokutana na kujenga dam eneo hili kunahitaji Environmental Impact Assessment ya hali ya juu. Uwepo wa machine kubwa, wafanyakazi lukuki, nk katika eneo hili wakati wa ujenzi kunahitaji mipango ya hali ya juu ili kuzuia poaching nk.

Ni mradi mzuri na naamini unahitaji kupewa "push". One complete the minimum amount of power that will be produced is 1500MW!
 
Ulikuwa mradi kabambe mwishoni mwa miaka ya 70 wa umeme na umwagiliaji maji ktk Bonde la Mto Rufiji na kama ungekamilika tusingekuwa na matatizo ya umeme hapa nchini na pia kufilisiwa kutokana na mambo ya emergency power kama ilivyo sasa.

Ulikuwa chini ya RUBADA (bado shirika hilo la Umma lipo) na ulikuwa unafadhiliwa na shirika la maendeleo la Norway - NORAD. Ulisimama wakati tuliamua kupigana na Idi Amin na inasemekana kuna fedha zilichotwa kutoka mradi huo na kupelekwa vitani.

Kuna habari kuwa mradi huo unafufuliwa tena, lakini hii ni maneno zaidi ya wakubwa kuliko vitendo, kikubwa ni kwamba wakubwa hao watakosa asali itokanayo na miradi ya umeme wa dharura.
 

Stieglers Gorge (Stigo) ni maporomoko ya maji kwenye mto Rufiji. Maporomoko haya yapo eneo liitwalo Kibesa ndani ya Pori la Selous. Na sisehemu ambayo mito mitatu inakutana na kujenga dam........if there's a dam anyway
 
Environmental Impact Assessment ilionyesha mradi huu una hasara kuliko faida. Na mimi nakubaliana nao.

Amandla........
 
Zungu Pule said:
Stieglers Gorge (Stigo) ni maporomoko ya maji kwenye mto Rufiji. Maporomoko haya yapo eneo liitwalo Kibesa ndani ya Pori la Selous. Na sisehemu ambayo mito mitatu inakutana na kujenga dam........if there's a dam anyway
Hakuna maporomoko katika Stieger's Gorge. 'Gorge' siyo "Water Falls."
 
Mkuu Kipunguni,

Mimi sio mtaalamu na wala sikuhusika na mradi huu lakini nilichosikia ni hiki:

1. Bwawa lingefunika sehemu kubwa tu ya hifadhi ya Selous. Kwa kufanya hivyo tungepoteza utajiri mkubwa wa viumbe, mimea n.k. vinavyoshamiri humo.

2. Kwa kuzuia flow ya mto Rufiji, mradi ungepunguza kwa kiasi kikubwa virutubwisho vinavyobebwa na mto kwenda kwenye Rufiji Delta. Hii ingekuwa na athari kubwa kwa mikoko, samaki na viumbe vingine vyote vinavyo shamiri kwenye delta hiyo.

3. Maji yanayotoka katika Dam hiyo yangekuwa na temperature tofauti na ilivyo kawaida. Hii nayo ingeathiri uhai wa viumbe vinavyotegemea mto huo.

4. Bwawa lingejaa tope kwa haraka kiasi kwamba baada ya muda si mrefu sana, uzalishaji wa umeme ungeathirika.

5.Palikuwa na hisia kubwa kuwa mabwawa makubwa yanasababisha kuongezeka kwa matetemeko ya ardhi. hali hii imeanza kutokea China ambako walipuuzia ushauri na kujenga mabwawa makubwa.

Yote haya ni irreversible. Tukishaharibu eco-system ya eneo hilo ndiyo basi. Kwa mtaji huo, mradi hauna tija kwa taifa letu na vizazi vitakavyotufuata.

Amandla.........
 

Usilete masuala ya kusikia mkuu; kama ni kusikia tu, hata mie nimesikia kuwa hiyo tathmini ya mazingira ilitolewa kisanii tu ... ili mradi usifanyike na wakubwa waendelee na mipango ya umeme wa dharura.
 
Usilete masuala ya kusikia mkuu; kama ni kusikia tu, hata mie nimesikia kuwa hiyo tathmini ya mazingira ilitolewa kisanii tu ... ili mradi usifanyike na wakubwa waendelee na mipango ya umeme wa dharura.

Mradi huu si wa jana au juzi. Mradi huu uliwekwa kapuni zaidi ya miaka ishirini iliyopita (wengine wa humu walikuwa hawajazaliwa). Hiyo tathmini ilifanywa na serikali ya Norway. Wao walikuwa ndio waufadhili na wao ndio walijitoa. Hayo ya umeme wa dharura unaozungumzia hayakuweko.

Badala ya kutafuta mchawi basi eleza kwa nini unadhani madhara niliyoyaelezea ni ya kusadikika!

Nakuwekea hapa chini ripoti kuhusu matetemeko ya ardhi katika eneo hilo. Au nayo unadhani ni usanii tu wa mafisadi? Kweli sikio la kufa halisikii dawa!


Amandla......
 

Hadithi nyingine za kusadikika hizo hapo juu.

Zimetoka hapa Report of the Technical Consultation on the enhancement of small water body fisheries in southern Africa - Harare, Zimbabwe, 25-29 January, 1993

Si kila kitu tunachoshauriwa ni kibaya. Mara nyingi adui yetu mkubwa ni sisi wenyewe. Hatuambiliki.

Amandla........
 
Fundi M:

Tu-provie authenticity ya hiyo ripoti. Pili, karibu mabwawa yote ya umeme -- Kidatu, Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu yamo katika hiyo EA Rift Valley System, na hivyo katika volcanic/erathquake activity region. Yanadunda hadi leo.
 
Fundi M:

Tu-provie authenticity ya hiyo ripoti. Pili, karibu mabwawa yote ya umeme -- Kidatu, Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu yamo katika hiyo EA Rift Valley System, na hivyo katika volcanic/erathquake activity region. Yanadunda hadi leo.

Unajua maana ya scale? Installed capacity ya mabwawa yote nchini ni 561 MW. Kidatu 200MW na Mtera 80 MW. Stiegler wanazungumzia 900MW!

Sina haja ya kukuthibitishia chochote. Hata ningetaka, nitafanyaje kwenye www? Ni uamuzi wako kuamini au kutoamini. Makes no difference kwangu.

Amandla.......
 

Kwa hiyo twende NYUKI (Nuclear) tu.
 
Stieglers Gorge (Stigo) ni maporomoko ya maji kwenye mto Rufiji. Maporomoko haya yapo eneo liitwalo Kibesa ndani ya Pori la Selous. Na sisehemu ambayo mito mitatu inakutana na kujenga dam........if there's a dam anyway

Stieglers Gorge ni nini hasa?--Stieglers Gorge ni mpalio mwembaba unaopatikana kwenye bonde la mto Rufiji, kilomita 374 toka jijini Dar es salaam. Kwa utafiti uliowahi kufanyika mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini [ 1978-1980] kwa ushirikiano wa RUBADA [Rufiji Basin Development Authority] na M/s Norplan/Hafslund, ilionekana kwamba mradi wa Stieglers Gorge una uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme mwingi kwa njia ya maji [Hdro-power] zaidi ya umeme ambao Tanzania ilikuwa ikihitaji katika miaka hiyo.

Matokeo ya utafiti huo pia yalionyesha kwamba, mpalio wa Stieglers una uwezo wa kuhimili mitambo mitatu mikubwa ya kuzalisha umeme [3 power stations]. Mtambo 'A' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia nne (400MW) ambao ungefungwa upande wa kaskazini mwa bwawa [dam]. Mtambo 'B' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia nane (800MW) ambao ungefungwa upande wa chini ya bwawa, na mtambo 'C' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia tisa (900MW) ambao ungefungwa upande wa kusini mwa bwawa. Jumla megawati elfu mbili mia moja [2100MW].


 

Attachments

  • Stiglers.jpg
    149.8 KB · Views: 113
Kumbe tunateseka na joto lote hili na giza nene la mgao wa umeme kutokana na kazi ya mafisadi na viongozi wala rushwa? Wallahi nchi hii itakuwa masikini milele...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…