Manuell
New Member
- Aug 26, 2022
- 3
- 1
Huyo ni mjusi/Dinosaur anayeamika kuishi Tanzania miaka mingi iliyopita ambaye kwa sasa mabaki yake yamehifadhiwa katika Makumbusho nchini ujerumani. hio ni moja kati ya maelfu ya kazi za kisanii, mabaki ya viumbe hai vilivyoibiwa katika kipindi cha ukoloni.
katika kipindi cha ukoloni ukiachana na biashara ya utumwa, unyanyasaji wa waafrica, wizi wa maliasili iliyokuwepo na vinginevyo kemkem, wakoloni walichukua/waliiba vitu vingi sana zikiwemo kazi za sanaa ambazo zilitumika kama vifaa vya ibada za jadi au viashiria vya tamaduni za makabila mbalimbali ikiwemo Vinyago, vito, mafuvu ya babu zetu, nguo za asili na vifaa vingine vingi sana na kuvipeleka nchini mwao, Ripoti ya wataalamu wa historia kusini mwa jangwa la sahara Wanasema 90% ya kazi za sanaa kutoka africa zimehifadhiwa nje ya bara la africa(ULAYA), huku zikihifadhiwa katika makumbusho mbalimbali, viashiria hivi vilitumiwa na wazee wetu wa kale katika maisha yao huku vikichukua nafasi kubwa katika imani na maisha yao.
Hivi karibuni tumeshuhudia ufalme wa ubelgiji wakirudisha kinyago katika nchi ya DR Congo huku ikiaminika wamerudisha kimoja kati ya artifact/ kazi za kisanii zaidi ya elfu 30 vikiwa bado chini ya makumbusho nchini ubelgiji, wizi huu ulifanyika chini ya tawala za kikoloni na bado unaendelea kwa kuvifungia nchini mwao ilhal nchi za africa zipo huru, swali la kuuliza ni je HUU NI MUDA SAHIHIHI KUVIRUDISHA AFRICA?, na JE SISI WAAFRICA TUNAJITAHIDI KIASI GANI KUHAKIKISHA MALI ZAILIZOIBIWA ZINARUDISHWA NYUMBANI?.
Africa kabla ya ukoloni ilikuwa na maisha yake, dini, utamadduni mila na desturi mbalimbali na viashiria hivi vya kazi za kisanaa vilitumika katika masiha ya babu na bibi zetu, lakini sasa asilimia kubwa ya vitu hivyo vya thamani vinavyoutambulisha Uafrica watu vimehifahiwa nje ya Africa huku tukiwa hutujui chochote kuhusu maisha ya wazee wetu wa kale, hii kwangu ni cultural genoside kwani tumekumbatia utamaduni wa wakoloni huku utamaduni wetu ukifichwa katika makumbusho za ulaya, inasikitisha kuona leo makumbusho za kama nchi ya Tanzania na nchi za Africa kwa ujumla, zikiwa na historia ndogo kushinda makumbusho za ulaya zilizo na stolen artifact zikibeba historia kubwa ya waafrica.
JE TUWAPELEKE WATOTO WETU WAKAJIFUNZE KUHUSU UTAMADUNI WA AFRICA ULAYA?
wito wangu kwa serikali na jamii nzima Afica ni muda wa kupiga kelele vitu hivyo virudishwe, tusikae kimya juu ya wizi huo nikirudi nyuma kidogo mwalimu Nyerere alipokuwa akizungumza na mwanahabari alitoa mfano wa koti akizungumzia kuhusu uhuru mfano ule unatukumbusha leo juu ya vitu hivyo kwamba ni vyetu haijalishi wao wanaonaje juu yetu ila kama ni vyetu ni muda warudishe.