STOP BARRICK GOLD CAMPAIGN - Wabunge Simameni!

Bado kuna kikao kinaendelea sasa kati ya timu ya Balozi na Barrick wakikutana na Mhe.Ndesamburo na kikao kinaendelea kwa mujibu wa taarifa zilizonifikia hivi punde.
 
Bado kuna kikao kinaendelea sasa kati ya timu ya Balozi na Barrick wakikutana na Mhe.Ndesamburo na kikao kinaendelea kwa mujibu wa taarifa zilizonifikia hivi punde.

Ndesamburo inabidi aonyeshe msimamo wa kizalendo, siyo siri ninawaamini wabinge wa upinzani kuliko chama tawala. Hawa wazungu hawana aibu kabisa, kwao maisha ni bora kwa kila mwananchi sisi tukitaka kujikwamua wanatupiga changa la macho na kutoweka na utajiri wetu.

Halafu inavyoonyesha huko bongo, watanzania wenye madaraka wanauwezo mdogo kuliko wasio na madaraka, haya yanakuwaje?
 
Hawa jamaa wamejipanga na ni jukumu letu pia kujipanga kwani la sivyo watatufunga bao la kisigino, kuna taarifa kuwa serikalini wamewaambia kwa waende wakawasiliane na wabunge kwani wao serikali hawana haraka ila bunge likiamua kuwa mapendekezo yapitishwe basi hawana budi kuchukua agizo la bunge ,ila kama bunge likiamua vinginevyo basi watafuata maagizo ya bunge.
 


Hata maandamano pia ni lobbying. Sio kila lobbyist lazima awe na tai na timu yake ya wataalamu. Maandamano dhubuti yana nguvu kushinda independent lobbyist yeyote. Kumbuka hii ni nchi ya watu na sauti za wenye nchi lazima zisikilizwe. It will be very difficult to simply dismiss or disregard well organised, coordinated and unified voices.

Maandamano have been proven to do just that throughout history
 

mungu ibariki tanzania, hao wameshatupiga bao la kisigino kabisa mie nakwambia, wabunge wengi wa chama tawala wakipelekwa mzungu huwa wanacheka mwisho(lugha) na sijui kama kawahaidi kuwapeleka canada kutembelea bunge la huko ndiyo kabisa.
kinachonishangaza mimi yuko wapi mh zitto si alikuwa kwenye kamati ya madini,kimya.

wapalestina toka udogoni mwao huwa wanaambiwa na wakubwa wao mabaya wanayofanyiwa na waisrael na matokeo yake huwa tunaona vijana wadogo wanajilipua. viongozi lazima mjuwe kwamba hizi kelele tunazopiga hapa haziishii tu hapahapa,taarifa zinaenea kote,ndiyo maana watu wanathubutu kuwazomea na kuwaita mafisadi, tunaonyesha dalili kwamba tumechoka kutendewa mnayotutendea kwa AMANI, sasa kama amani za kuzomewa mnazipuuza hipo siku ataanza mtu kupiga gari mawe, nayo kama yatapuuziwa wala sitamani ni wapi tutaelekea. nawaomba tu mkome mkome tena mkome na haya mnayotutendea.
 

Mkuu Zee maneno mazito sana haya, hapa tupo ukurasa mmoja, lobbying sio crime kwa sababu hata UN unaweza ku-lobby, tatizo ni je Tanzania tunajua namna ya kusimama kidete kusiammia masilahi yetu mbele ya wazungu, je do we stand a chance?
 
Kinadharia, wabunge ndio walitakiwa wawe watetezi wetu. Lakini wabunge wa Tz waliojaa ubinafsi, nidhamu ya woga kwa chama, na wengine wa viwango vya Chitalilo; inakuwa vigumu kuwategemea kusimama kidete kutetea maslahi ya nchi.

Kwao(wabunge), bora wakaialika timu ya mpira ya vijana(copa coca-cola blah...blah), au zee komedi bungeni.
 
barrick wana uwezo wa kumwaga pesa na opportunities nyingi sana kwa wabunge wetu....na hicho ndicho kinachonitisha hasa ukizingatia kuwa wabunge wengi hawajui sababu ya kuwepo kwao bungeni
 
Kama za Rostam tu zinawatia kiwewe viongozi wetu, itakuwa za wazungu toka nje?

Yaani hii generation ni hopeless kabisa!
 
Hawa jamaa naambiwa kuwa wpo bize sana huko bungeni na wanakutana na kila mbunge,kinachotisha ni kuwa wanakutana na Mbunge mmoja mmoja sasa huenda huko ndio wanawaahidi kitu ama safari ama kamradi ka maji si unajua tena wabongo na mzungu?

Lazima kupiga kelele this time.
 

Ooooh! Hapo kasheshe; wengine watapatikana kwa mtindo huu!!
 
Hapo kuna kazi kubwa, inabidi tutumie Mugabeism kwa Wabunge wetu kutumia syle ya Mugabe liwalo na liwe!

Lakini pia ni ujumbe kwetu na kwa Wabunge kuwa Wawekezaji ndiyo wanaofaidi zaidi raslimali za nchi yetu kuliko sisi na ndo maana huyo Balozi ame-panic.

Wabunge kumbukeni hili:

"Watanzania Si Mabwege Tena" Dk Mwakyembe.
Wananchi tunafuatilia kwa ukaribu masuala ya mustakabali wa nchi yetu
 

Barrick na canada Hoyee.Tusaidie sisi wanyonge.Mlio wengi humu JF muko huko ulaya mambo safi.Je mimi wa hapa Nyamongo nikale wapi.Rudini hapa TZ muone jaa ilivyo kali.
 

Koba,
Ukiangalia mifano ya Zambia na Congo hakuna cha pande zote kukubaliana.
Leo tukipata serikali makini isiyo ya CCM kuna uwezekano mkubwa wa mikataba hiyo kuwa abrogated kwa sababu halali kabisa, (ie: ilisainiwa kwa hongo, etc etc) Hakuna sababu ya kumshirikisha Barrick eti tujadiliane upya. Kwa mujibu wa Mzee Bomani, baadhi ya mikataba ililetwa nchini imeshaandikwa kabisa na hao wawekezaji na sisi tulichofanya ni kuweka saini tu. Sasa mikataba kama hiyo haina haja ya kukubaliana juu yake.
 

Ama kweli duniani wawili wawili...Kama ambavyo sasa tumeshajuwa kuwa Sinclair ndio modern Karl Peters na apparently nothing has changed kwa watawala wetu kwani pia tunao modern chifu mangunguz!

Kama wabunge hawatasikiliza kilio cha wananchi mbona nitai copy an paste ile signature ya Nyani Ngabu na kuitumia RASMI!
 
Hata kama bei ya dhahabu ni $1000 sisi hatutapata $30 ila ni 3% ya $300 ya bei wakati wa kusaini mikataba. hawaangalii bei kupanda. nadhani moja ya mapendekezo ya kamati itakuwa ni mrahaba kwenda sambamba na bei kupanda.

Kweli tutafute njia ya kutoburuzwa na hawa wazungu
 

Hapo ndipo kwenye mzizi mkubwa sana.
 
Nita shangaa sana kama wabunge wetu watakubali kurubuniwa this time pamoja na kelele zote zinazo pigwa toka kila kona ya nchi na wakati mwingine zikipigwa na hata wao wenyewe!

Naamini kwamba hawata kuwa tayari kurubuniwa na viperemende kwa kuliangamiza taifa letu!

Huu ndio wakati pekee (Golden chance) ya kuweza kurekebisha unyonyaji ambao umekuwa ukiendelea kwenye uchimbaji wa madini yetu, Litakuwa ni jambo la ajabu sana kama serikali yetu ambayo ndo imekuwa ikiwalinda hawa wawekezaji wezi, kwamba safari hii imeisha jitoa na kuwaaambia kweli kwamba wenye mamlaka ni bunge, then wabunge wetu ndo mtuangushe!

Si kwamba wananchi wenu hatuta waelewa bali hata Muumba wetu atawalaani! please please nawasihi kwa jina la Mungu wetu, (na hata miungu yote ya wasio amini )msikubali kamwe kwanamna yoyote ile kurubuniwa!
 
Mchakato wa kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa unawanufaisha watanzania unaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali na huyu balozi na ujumbe wakew wako kwenye state of panic kwa taarifa nilizo nazo mpaka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…