Misaada ambayo Tanzania imewahi kupewa tangu uhuru kama ingetumika vizuri nchi ingekuwa mbali sana inavyoelekea nchi hii haina vipaumbele{priority}.Tatizo linaloikabili nchi yetu pia ni ukosefu wa uwazi katika matumizi ya fedha za misaada tunazopewa na nchi wahisani.Fedha nyingi tunazopewa kwaajili ya miradi ya maendeleo zinatumika kwenye semina,kongamano,warsha & nk,tuchukue mfano wa mradi umwagiliaji.Asilimia 50% ya fedha zitatumika kwenye semina,20% usafiri {L / Cruiser VX & GX,Prado,mafuta & vipuli},20% technical {wataalamu kutoka nchi iliyotoa msaada}& 10% zitawafikia wananchi.Mara nyingi ninaposikia Tanzania imepata msaada wa mabilioni kutoka nchi wahisani picha ya semina na makongamano kwa wigi inanijia kichwani.
Misaada pia imetulemaza kwa kiasi kikubwa.sina figures kamili lakini waziri wetu wa fedha anaposoma budget nadhani kuna mahali anatamka bila aibu kabisa kwamba budget hii ina nakisi ya 40 % ambayo nchi wahisani wanategemewa kuchangia nakisi halafu nchi ambazo zimetoa ahadi ya kuchangia pengo la budget zinatajwa moja baada ya nyingine waheshimiwa wabunge nao hawako nyuma kushangilia kwa kupiga meza!.Mahali ninapoishiwa nguvu kabisa ni pale serekali inapoagiza magari ya kifahari kwa mawaziri,wakuu wa mikoa,makatibu wakuu,wakurugenzi & makamishna.Land Cruiser moja thamani yake ni zaidi ya Tsh 100 milioni kwa mikoa 22 ni sawa Tsh 2.2 bilioni hii ni hesabu ya wakuu wa mikoa tu bado makatibu tawala wa mikoa nao wako 22 tena siku hizi wamezalisha cheo cha katibu tawala msaidizi wote hawa wanastahili kutumia magari ya kifahari.Sijui kuna tatizo gani kama mkuu wa mkoa au waziri atatumia Suzuki,Land Rover au Land Cruiser hardtop.Nimezungumzia kipengele kimoja cha matumizi ya magari tukienda katika kila kipengele utagundua Tanzania hatuna haja ya kuomba misaada.Fedha za manunuzi ya magari ya kifahari pekee yake kama zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule za sekondari hakuna mtanzania atakayelazimishwa kuchangia ujenzi wa hizi shule za kata.
Ngongo nakubaliana na maoni yako mazito...Nakubaliana kuwa misaada isimamishwe.
Hivi tukiangalia kiundani nani anamsaidia nani?
I mean honestly...Wanachochukuwa na wanacholeta kipi kina thamani kubwa zaidi ya kingine?
Mimi nadhani sisi ndio tunatowa misaada na malipo yao nadhani ni kidogo na hivyo ni budi kuyasimamisha.
Ila hatuwezi kufanya hivyo ni hadi uongozi huu wa bora liende uondolewe...I mean mapinduzi ni lazima otherwise hatuendi mahali na hii ni guaranteed.
Saa nyingine ni bora kuvunja na kujenga upya badala ya kurepea tu.
Ufa tulionao ni mkubwa sana and so we need a new direction in whatever means neccessary.
Kwani tumeshajiuliza kuwa nini hasa mikakati ya muda mrefu ya misaada hiyo ambayo tumekuwa tukipokea mara baada ya uhuru wa bendera?
Ama misaada ndiyo imekuwa utamaduni na biashara?
No wonder NGO zimekuwa deal na wasomi wanazianzisha tu huku wakisubiri kuzikinga pesa za misaada ya UKIMWI,malaria,homeless kids etc.
Tujifunze sasa watanzania na tuelewe na kuzisoma jamii nyingine zinazotunzunguka na tunazo interract nazo...Je ni kweli watu hao wana nia ya kusadia ama ni mtandao wa kifisadi duniani kote kati ya mafisadi dhidi ya raia masikini?
Hatuhitaji misaada tunahitaji viongozi wapya wenye fikra mpya za kimapinduzi za kutupeleka in a different direction ....Tunachohitaji ni Positive ideas,better techology,Fair trade na baada ya hapo mambo safi.
Tukipewa share yetu fair kwenye biashara na kuwapatia wananchi kazi basi tutatumia pesa zetu kununuwa hayo madawa,neti na kondom kwa pesa zetu waache kutuyeyusha hao wakoloni na manyapara wao mafisadi.
Time is over.