Stop Foreign Aid to Tanzania Campaign!!

Hatimae misaada imesitishwa, Marekani imetulazimisha kuwaza , kupanga, kulipa kodi na kutumia kodi zetu vizuri kugharamia maendeleo yetu wenyewe
 
Haya sasa Maccm ni wakati wa kuyauza yale mabasi ya kijani/njano, bajaji na bodaboda mlionunulia na pesa za misaada kutoka kwa Trump kwa ajili ya kusomba raia kuwapeleka kwenye mikutano yenu ya kampeni. Bata wahed!
 
Sijui ni ujinga au ni kitu gani.

Kama wananua gari moja cash kwa ajili ya RC, DC, RAS,DAS na makada wengine wa Lumumba $30,000 likifika bado kuna pesa ya service na mafuta huku kuna watu bado vijijini huko wanakunywa maji kutoka chanzo kimoja na mifugo yao , wanafunzi hawana mahali pa kukaa darasani, wengine hawatoshi darasani ,miundombinu ya barabara bado mbovu ila kwenye tafrija, warsha na mikutano watu wanakuja wamependeza kujadili vitu visivyo na tija lazima ujiulize kama kuna viongozi timamu.
 
Kuna mwanasiasa nimemsikia anasema "maendeleo yanasababisha matatizo, mfano wingi wa vyuo unaongeza vijana wasio na ajira"...sina hakika kama ni yeye ama ni AI
 
Inasikitisha hii nchi watu wenye akili timamu wamekuwepo wakati wote lakini hawataki kufanyia kazi maoni yao, wakati umefika kazi ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…