Stori 10 na Kategile Mathias(21)kutoka Sikonge-Tabora, Mchezaji wa mpira wa miguu

Joined
Oct 18, 2015
Posts
11
Reaction score
0
Anaitwa Kategile Mathias(21)kutoka Sikonge-Tabora ni mchezaji wa mpira wa miguu(kipa)na hizi ni stori zake 10[emoji116][emoji116][emoji116]
[emoji835]"sijawahi kudanganya umri...wachezaji wengi wanadanganya umri ili wacheze soka muda mrefu...nashauri tusidanganye umri wetu kwa sababu tunawanyima nafasi wadogo zetu wenye ndoto ya kucheza"
[emoji836]"mpira wa bongo unahusisha ushirikina sana...siwezi kusahau mechi kati ya red star na tumbaku fc ilikua na ushirikina mwingi mno,mvua ilinyesha kubwa sana red star tukafungwa goli moja baada ya goli hilo mvua ikakata palepale na matokeo yakabaki hivohivo"
[emoji835]"role model wangu katika soka ni Aishi Manula kipa wa Simba sc club"
[emoji836]"sipo katika mahusiano bado...ni kweli mapenzi huathiri perfomance ya mchezaji kama atajikita zaidi huko na kuacha mazoezi"
[emoji837]"nilikua na timu ya mkoani,tumemaliza kufanya mazoezi jioni kocha akataja wachezaji watakaosafiri na timu kwenda singida...mimi nikiwa mmoja wa wachezaji 20,ila kesho yake asubuhi nilishushwa kwenye gari na mabegi yangu,viongozi wakaniambia nibaki kambini,sitasahau tukio hili"
[emoji838]"wachezaji wengi wakipata timu huridhika na kujisahau wakati mchezo wa mpira ni kupambana wakati wote...mwisho hufeli na kurudi nyumbani"
[emoji837]"tulichukua ubingwa wa ligi ya mkoa wa Tabora"(sitosahu)
[emoji838]"mafanikio ni madogo sana...ninajitahidi ili niweze kupata mafanikio makubwa zaidi"
[emoji835]"ligi yetu haina mdhamini pia viongozi wetu sio wakweli katika kuendesha timu"(changamoto)
[emoji836]"malengo yangu mwaka ujao(2019)ni kucheza ligi kuu na baada ya hapo nje ya nchi(malengo)....vijana tupambane na kujituma zaidi ili tuweze kutimiza ndoto zetu"(ushauri) MAHOJIANO NA JOSEPH ERNEST

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Sasa unachezea timu gani? Timu ya WATUMISHI kata ya Tutuo Sikonge Tabora wanakukumbuka ssaana. Pia wanakuombea kila laheri katika harakati zako za mpira.
 
"malengo yangu mwaka ujao(2019)ni kucheza ligi kuu na baada ya hapo nje ya nchi(malengo)....vijana tupambane na kujituma zaidi ili tuweze kutimiza ndoto zetu"


Yupo team gani sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…