Man Middo tz
Senior Member
- Sep 9, 2020
- 182
- 279
STORI FUPI: JINSI YA KUTAFUTA FURAHA YAKO.
Alitokea mwanamke mmoja aliyevalia nguo za gharama sana, kwa kumtazama tu ilitosha kutambua kuwa ni dada wa kitajiri. Basi alienda kwa mwanasaikolojia akamwambia kuwa
“Sina furaha na maisha yangu nipo na huzuni, yani kiufupi maisha yangu hayana maana yoyote, Sioni umuhimu wa mimi kuishi”
Yule dada alionekana kukata tamaa kabisa, mwanasaikolojia akamtazama kisha akamwambia kuwa
“Ngoja nikamuulize Malietha akwambie ni kwa namna gani amepata furaha. Kitu pekee ninachohitaji kwako nikumsikiliza tu”
Mwanasaikolojia akamuita Malietha, alionekana mtu mzima kidogo, Malietha kazi yake ni kufanya usafi katika ile ofisi ya mwanasaikoojia. Basi yule dada akaja akaweka dekio lake kisha akakaa na kuanza kumueleza yule dada wa kitajiri stori yake.
“Mume wangu alikufa kwa kansa, miezi mitatu baadae kijana wangu wa pekee akafa kwa kugongwa na gari. Sikua chochote.. sikua na mtu yoyote aliyebaki… Sikuweza kulala.. sikuweza kula, sikuwahi kutabasamu kwa yoyote.
Nilifikiria hata kuutoa uhai wangu mwenyewe. Basi siku moja jioni, wakati narudi kazini mtoto wa paka alinifuata nyuma nyuma hadi nafika nyumbani, kwa kiasi nilikaonea huruma kale kapaka.
Nje kulikua na baridi sana, hivyo nikakaacha kaingie ndani. nikampa maziwa kidogo, nikashuhudia akayanywa yote hadi kusafisha sahani. Basi akaja kunusa mguu wangu kama vile anashukuru, kwa mara ya kwanza ndani ya miezi kadhaa, nilitabasamu.
Sasa hapo nikafikiri nikasema ‘Kama kusaidia haka kapaka tu kumenifanya nitabasamau, Inaweza kuwa kufanya kitu kwajili ya watu wengine kukanifanya niwe na furaha’
Hivyo siku iliyofuata nikachukua biskuiti na vitu vingine nikawapelekea majirani ambao wamelazwa kwa magonjwa mbali mbali.
Kila siku nilijaribu kufanya kitu kizuri kwajili ya mtu mwingine. Ikanifanya niwe na fuaraha sana kuwaona wao wakifurahi. Hadi leo sijui kama kuna mtu anapata usingizi mzuri na bora kama ninaoupata, Hivyo nimepata furaha kwa kuwapatia furaha wengine”
Pindi aliposikia hivyo yule dada wa kitajiri alilia, Alikua na kila kitu ambacho pesa inaweza kununua mfano gari, nyumba, nguo na vitu vingine vya gharama, Lakini alikua amepoteza vitu ambavyo pesa haiwezi kununua kama uhai wa mtu nk. Toka siku hiyo akaiga yale Malietha aliyofanya hadi kupata furaha.
FUNZO: uzuri wa maisha yako hautegemei ni kwa namna gani upo na furaha, ila unategemea ni jinsi gani wengine wanafurahi kwasababu yako. Furaha sio hitimisho ila ni safari. Furaha sio kesho, furaha Ni sasa. Furaha haitegemei mtu, Furaha ni maamuzi yako. Furaha ni wewe ni nani, Furah sio kile ulichonacho.
Wengi wanaamini kuwa na pesa ndio kuwa lakini kuna watu wanapesa na hawaijui fuaraha kabisa, Mshukuru Mungu kwa pumzi uliyonayo. Kuanzia leo hebu kuwa sababu ya watu wengine kufurahi, hebu kuwa sehemu ya watu wengine kupata tumaini.
@middotz_