Stori na gumzo kutoka vijiwe vya kahawa

Stori na gumzo kutoka vijiwe vya kahawa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Vijiwe vya kahawa nchi hii ni sehemu mojwapo maarufu ambayo mengi huzungumzwa na kujadiliwa yanayohusu siasa za ndani na nje ya nchi,historia mahusiano,dini, biashara, uchumi n.k.

Mambo yanayojadiliwa mara nyingi huegemea katika nadharia za kinjama(consipiracies theories), upotoshaji,uongo,ukweli ,mchanganyiko wa baadhi ya hayo au wa yote.

Jambo gani ulilowahi kulisikia kutoka vijiwe hivyo(ambavyo vinaweza kuitwa JF iliyo wazi/hadharani/mubashara) likakufikirisha, kukufurahisha, kukuudhi au kukuchefua?
 
Hayo ni maeneo maarufu ya wafuasi wa Mudy, ngoje walete feedback...

Mhudumu lete safari lager baridi nyingine...
 
Hio kahawa naona kama ina lewesha
Maana kabla watu wahawaja tumia wanakua poa ila wakisha tumia inakua tabu
 
kama unapenda wajue profile yako jichanganye vijiwe vya kahawa.
VIjiwe vya kahawa vina habari zote kuanzia kitaifa,kimataifa,hali ya hwa,uchawi,ushauri,nasahaa,waliofulia,kazi,michongo na n.k

TATIZO LA KIJIWE CHA KAHAWA:
*LAZIMA KUWE NA MJUAJI
hapa kuna yule mjuaji wa vyote au mjuaji jambo moja kama ni michezo,habari,dini,siasa,madawa,umri kwenda na n.k
*WASTAAFU NA WAZEE
kahawa ni kijiwe pendwa sana cha wazee wakijadili uzee wao.
*SIASA NA SIRI NYINGI
vijiwe vingi vinajua siasa ukiachana na vijiwe vingine na vijiwe vya kahawa vina wafuasi wengi wakila nyanja.ndio maana mambo yote yanaanza vijiwe vya kahawa.
*UONGO NA KUAMINISHA
ukiwa na akili fupi kijiwe cha kahawa wanakupoteza kwa story zao na mambo yao.
*KIJIWE CHA FITINA NA KUJUWA WATU
ukitaka kujua leo nani kafulia,nyumba inauzwa,kafumaniwa,malaya,mwizi,mchawi na n.k vyote utapata kijiweni.
*WALONZI NI WENGI
kijiweni kuna walonzi na watu ambao wamejichoka au chuki yani unatakiwa ufanane nao sio kujionesha utoboi.
*KIKOMBE CHA KAHAWA AKIWEZI KUKUAMSHA KIMAENDELEO
vijiweni walizikaji ni wengi yani ukipata buku basi ufikirii tena na ndio maana majobless na wasiotaka kazi wapo hapo.
*DAWA ZA MITISHAMBA KIJIWENI NDIO SEHEMU YAKE
mimi mwenyewe vumbi la kongo nimelijua kijiwe cha kahawa.ukiumwa usitegemee wakwambie twende hospitali bali utaambiwa miti shamba

wenye kuongeza
 
Huku Tanga kuna wazee wako kwenye vijiwe vya kahawa na kucheza dhumna lakini wana viunga vya minazi na nyumba za kutosha barabara za namba,wengine wana madau baharini! Hawana njaaa..kutwa nzima wako maskani..wakiamka wanaenda msikitini wanarudi!
 
Huku Tanga kuna wazee wako kwenye vijiwe vya kahawa na kucheza dhumna lakini wana viunga vya minazi na nyumba za kutosha barabara za namba,wengine wana madau baharini! Hawana njaaa..kutwa nzima wako maskani..wakiamka wanaenda msikitini wanarudi!
Wale wazee wengi wanaomiliki majahazi ya uvuvi Wana pesa sema wazee wa nyumba nyingi unakuta Wana wanawake wa4 🤣🤣 hawataki stress .


Kuna siku nilikuta kijiwe cha kahawa fulani wanaongea mpaka kingereza sio kwamba wasomi ila ni wazee sana walijulia kupitia mkoloni.
 
Back
Top Bottom