Phobia
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 1,156
- 1,819
MY STORY: Alinibebesha ujauzito Mama yangu akamakataa akafungwa miaka 30 kisa Dini.
Nilipomwambia Mama yangu kuwa nina ujauzito wa mwanaume ambaye si wa dini yangu, alikasirika sana. Aliniambia nisimwambie mtu yeyote na hakuna namna nitaolewa na huyo mwanaume. Wakati huo, baba yangu alikuwa Singida kikazi na sisi tulikua Dar, hivyo kila kitu nilikuwa naongea na mama kwa sababu kipindi hicho hata hakukuwa na mambo ya simu kama sasa. Mama alikua ndiyo kila kitu kwenye familia, kwakua alikua na kipato kikuba kuliko Baba hata ningeongea kitu na Baba isingesaidia, alikua akisema hapana basi wote mtaaka kimya, Baba alikua hana kauli.
Mwanaume wangu alikuja nyumbani kujitambulisha lakini mama alimkataa na kumwambia kuwa mimba niliyonayo si yake bali ni ya mwanaume mwingine, hivyo akae mbali na mimi. Kijana wa watu hata hakukubali, alihangaika sana kutaka kuongea na baba lakini mama aligoma na kumwambia kama ataendelea kunisumbua basi atamf*anyia kitu kibaya.
Mimi nilijua kama ni utani, mama yangu ninavyomjua hawezi kufanya kitu chochote kibaya kwa huyo kijana. Kipindi hicho mimi ndiyo nilikuwa nimemaliza chuo na huyo kaka yeye tayari alikuwa anafanya kazi, alikuwa ni mwalimu katika shule moja hapa jirani na mapenzi yetu yalikuwa ni ya muda mrefu hivyo tulishakubaliana kuwa tutaishi pamoja na kila mmoja atabaki na dini yake ila hicho kitu mama alikataa kabisa kukisikia.
Hata alipokubali kubadilisha dini, bado mama alikataa na kuniambia hakuna mwanaume anayebadilisha dini kwa ajili ya mwanamke, huyo anacheza na akili zako, atabadilisha leo lakini baadaye atarudi kwenye dini yake, sitaki hizo aibu mimi. Mama aliongea lakini mimi hata sikusikia, sikuwa sawa nikamwambia kaka yangu, yeye ndiye alinip*iga sana, tena maeneo ya tumbo ili mimba itoke, akaniambia hatumtaki huyo mtoto wako wa haramu hivyo kaa mbali na huyo mwanaume.
Kuona hivyo hakuna mtu anayenisikiliza nikaamua kutoroka nyumbani na kwenda kwa yule mwanaume. Sikujua ni kwa kiwango gani mama yangu alikuwa si mtu wa mchezo na hilo jambo. Baada ya mimi kutoroka tu, siku mbili baadaye polisi walikuja nyumbani, mwanaume wangu alikamatwa na kuwekwa ndani. Kosa lilikuwa nini? Niliambiwa kuwa kuna wanafunzi walimshtaki kuwa wana mahusiano naye, hivyo akakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la ub*akaji.
Kweli niliumia sana kwa sababu mama alinambia kama utaendelea kumng'ang'ania huyo mwanaume basi nijue kuwa ataozea jela. Alinambia salama yangu ni kuitoa hiyo mimba na nisimtafute tena huyo mwanaume. Niliweka msimamo kwa mwezi mzima na mwanaume alikuwa ndani, ndugu zake walishakuja na kumuomba mama msamaha lakini aligoma. Sijui alitoa pesa kiasi gani, kwani mama mbali na mbali na kipato chake, lakini alikuwa na cheo fulani na alikuwa anawajua watu wengi wakubwa hivyo ilikuwa rahisi kwake kufanya chochote.
Baada ya mwezi, nilimuonea huruma mwanaume nikaamua kutoa mimba. Nilianza kuhangaika kuhusu kuitoa, hakuna dawa sikunywa, hakuna sehemu sikwenda mpaka dawa za uchungu nilikunywa lakini mimba haikutoka. Nilianza kudhoofika, hali ilikuwa mbaya ndipo watu walimwambia mama kuwa nitak*ufa, muache mtoto azae. Kweli hakuwa na namna, alikubali kuniacha kuzaa kwa makubaliano kuwa hata nikijifungua sitasema kuwa mtoto alikuwa wa yule mwanaume na mtoto atakabidhiwa mwanume mwingine haraka haraka amma alinitafutia mwanaume mwingine nikafungishwa ndoa na mwanaume ambaye hata simjui vizuri!
Nilikubali lakini hatukuweza kumtoa mwanaume mahabusu. Kufika kule, kumbe kabambikiwa kesi nyingine akiwa ndani, si ile ya mama kumpeleka ndiyo kapewa kesi nyingine ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo ilikuwa haina dhamana. Kuna mtu walikutana naye mahabusu huko sijui katika kutaja, akamtaja kuwa naye alihusika, hivyo akaunganishwa kwenye hiyo kesi.
Ilikuwa kama utani lakini ndiyo hivyo, mwanaume wangu alikaa mahabusu kwa zaidi ya miezi 9 na baada ya hukumu alifungwa miaka 30. Kama utani vile, lakini siku ya hukumu ndiyo ilikuwa siku yangu ya mwisho kumuona. Nilikuwa nalia kila siku, mama aliniomba sana msamaha, lakini sikumwelewa. Baba alipokuja alijua kila kitu, alijitahidi sana kumsadia na hakuwa mkali kama mama lakini bado haikusaidia.
Mwisho, sikuwa na namna ilibidi nikubali matokeo. Niliolewa na kuishi maisha mengine na kwa namna fulani nilimsahau na kukubaliana na ukweli. Baada ya mwanangu kumaliza chuo mwaka jana, alianza kuulizia kuhusu baba yake, kuna maneno alisikia kuhusu ishu yangu akajua kuwa Baba aliyekua anamlea na kujua ni Baba yake hakua Baba yake, alikuwa na maswali mengi lakini sikuwa na majibu.
Sijui ni nani alimwambia lakini mwezi uliopita alifanikiwa kufika mpaka nyumbani kwa baba yake. Aligundua kuwa alishamaliza kifungo chake lakini baada ya kutoka jela, hakuishi muda mrefu, alitoka akiwa amechoka na maisha na miezi 3 tu alifariki dunia. Mwanangu alijua kila kitu kilichotokea kwani ndugu zake walimweleza hivyo mpaka sasa hataki kuongea na mimi.
Mama yangu ni mtu mzima sasa, hata kumbukumbu ameanza kupoteza, sijui ni laana au nini lakini amekuwa mtu wa kujisaidia hapo hapo, ni mtu wa kusaidiwa. Natamani hata kwenda kuliona kaburi lake lakini sijui hata ndugu zake wataniambia nini! Natamani mtoto wangu ajue ukweli kwamba nilimhanagikia Baba yake ila bado najilaumu kwa yote yaliyotokea.
MWISHO