Stori ya muvi ya War Horse 2011

Stori ya muvi ya War Horse 2011

8ATP

Senior Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
167
Reaction score
217
War Horse 2011
Farasi wa Vita.
Hichi kisa cha War Horse

1912 Devon, England jamaa-Ted ananunua Farasi mnadani kwa mkwara anamu-outbid mwenye nyumba wake, watu wote wanamshangaa mbona Farasi sio wa kazi. Nyumbani mkewe anashangaa, maamuzi gani Ted-mumewe amefanya, kama vipi bora arudishe tu. Dingi anakomaa anampa mtoto wake (Albie) amufundishe kazi ya kulima. Albie anamfundisha na baadaye Farasi na yeye wanakua marafiki. Wanalima kwa Farasi yule yule, waliombeza hawaamini mpaka mwenye nyumba anakasirika maana alimtaka sana yule Farasi mnadani. Shamba walolima mambo yapo fresh wanasubiri wavune wamlipe landlord. Duh!! ng'ombe wa masikin hazai, yanatokea mafuriko mazao yanaharibika. Ted anafanyaje?

1629282814670.png


Mungu mkubwa inatokea vita kati ya German na England msimu huo huo-1914. Ted anaamua kumuuza Farasi jeshini apate kodi ya kumlipa mwenye nyumba, Albie anakasirika anaona bora aende yeye sababu Farasi anampenda, lakini dogo ni under 18.
Basi inabidi akubali, anamfunga Farasi kitambaa chekundu kama kumpa bahati anavyokua vitani. Kaptain wa jeshi anamuahidi dogo Farasi atamurudishia.

Vitani mapambano ya kwanza tu captain kikosi chake kinapoteza yeye mwenyewe anauwawa lakini Farasi anapona anaangukia mikononi mwa jeshi la German-wanaanza kumtumia wao. Yaani Farasi alokuwa wa England anatumika na jeshi la German.

1629283137461.png


Jeshini upande wa German, madogo waoga wa kijerumani wanatoroka kwa kutumia Farasi yule yule wa Ted. Wanakwenda jificha kwenye shamba la babu Emilie. Wanajeshi wanawapata madogo bila kuwaona Farasi waliotoroka nao, hafu wanapigwa shaba kwa usaliti. Wanaokotwa na Emilie.

Wanajeshi wakawa wanaenda pale kwa babu kuchukua mazao shambani, ila Emilie aliwapenda Farasi akawa anawaficha chumbani wajerumani wasiwachukue. Ila walivyorudi tena kwa mara nyingine wakawaona Farasi wakawabeba, babu akalani sana akabaki na kitambaa kile chekundu.

Farasi anarudi vitani tena kwa mara nyingine upande wa German, 1918 The Somme, Ufaransa kikosi cha England na Albie ashakua, akiwa na matumaini ya kumpata Farasi wake. Vitani Albie anapigwa gesi macho yanapata upofu.

Mapambano yanakua makali Farasi anapata upenyo anakimbia huku na kule kujiponya anasa kwenye senyenge uwanja wa vita. Wanajitokeza wanajeshi wawili kutoka England na German wanakata waya kumsaidia mwisho wanarusha shilingi nani amchukue. Anachukua mwanajeshi wa England. Bahati.

Kambini upande wa England unatokea mzozo sehemu ya huduma ya kwanza alomchukua Farasi anataka anataka atibiwe mwingine anasema wampige shaba afe vidonda havitibiki. Albie alokuwa kipofu, anapiga muluzi Farasi anasikia. Albie anaomba wasimuue na anawatajia alama za Farasi wake.

1629283486899.png


Vita 1918 vinamalizika Jeshi linaamua kupiga mnada Farasi wote kufidia gharama za vita, babu Emilie anasaikia kuna Farasi wa maajabu anauzwa. Anaenda anaona ndo yule alowahi kuishi kwake anaweka dau kubwa ili wengine washindwe,anamchukua akampe zawadi ya hio mjukuu wake.

Albie anamkosa tena Farasi wake, ila anambembeleza huku Farasi akiwa hataki kuachana naye tena. Mzee anamuulizia juu ya kile kitambaa chekundu Albie anampa kisa chote babu anamuonea huruma anamuachia Farasi wake.

1629283368337.png

Na hiyo ndo muvi WAR HORSE
Director Steven Spielberg, kaicheki ina kisa poa sana.
 
Back
Top Bottom