Story: Chini ya Bahari

Story: Chini ya Bahari

Binadamu Mtakatifu

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2021
Posts
4,226
Reaction score
8,879
Part 1

Mvua inanyesha aridhi nayo chapachapa dongo jekundu natoka kwenda kusaka, mguu mosi mguu pili mpaka kunako shamba naanza kuchimbua ili kupanda zangu karanga,

Namaliza kipande pekee baba yangu alichonikwezea japo si haba napata kitu mdomoni, hii ni baada ya kufiwa na wazazi wangu tulizaliwa sita watano hatunao tena mimi ni wamwisho na maisha yangu ni mtihani sugu ndio mshahara wangu sio kwa mpini ule

kabla ya haya maisha wala hayakutupenda mama yangu mzazi alikwisha fariki na Mwanamke wa kambo aliiteka nafasi, yalianza manyanyaso jasho na shari yalikuwa ndio ndugu wa kweli

Baba naye alizuzuliwa na kipochi cha katili wala hakunijali vipigo kila siku, siku iliwadia ambayo Mungu alinitunuku zawadi ya maisha dhidi ya mateso yangu, nilitumwa ahsubuhi kwenda kuchimba mihogo nilifanya kwa imani japo siuwa na nguvu kutoka kwa lishe duni mwilini

Niliitua nyumbani mtoto nisie na hatia ilipachikwa jikoni na kisha ikaiva nilitupwa shambani bila hata ya kitu kinywani ili tu nisionje kisa waliwekea na nazi, hawakujua ni heri kwani nilipewa nafasi aliifakamia wasijue ingalipo na sumu

nilidondoka shambani kwa njaa kali nilizinduka kitandani watu wamenijalia, nilipewa supu na maziwa ya kutosha ilikuwa ni dodo chini ya mchongoma nilikula nilikula wala sikuzubaa ili yule mwovu asiniwahi akamwaga

Jiandae tukazike ilikua kauli tata kwamba mimi nipo hai wakanitumbukize? la hasha nilipewa mkasa wa ndugu zangu nyumbani wala sikusononeka kwani nilitua mizigo

siku zilisonga ndugu wakajisevia waliniachia shamba na kibanda kinachovuja yote ni maisha na ndipo ninapopambana, kuiweka future sawa

Naitwa Issa kijana mshaarabu kijana niliyepanda mbegu ya huruma moyoni ila maisha yananipigia kushoto ni haki kuzaliwa ila ningelipewa uamuzi basi nisingelikuja huku

ITAENDLEA
 
Naomba nijue Ina mizinguo au bandika bandua ili nisipate huzuni kwa kuikosa?!
 
Back
Top Bottom