Story: Hekima ya Nasoro

Story: Hekima ya Nasoro

BoyHimself

Member
Joined
Mar 27, 2022
Posts
29
Reaction score
23
๐Œ๐œ๐ก๐ž๐ณ๐จ ๐ฐ๐š ๐’๐š๐ซ๐š๐Ÿ๐ฎ ๐’๐จ๐ค๐จ๐ง๐ข.

Kila siku Nasoro alikuwa akienda kuomba msaada sokoni, na watu walikuwa wakimdhihaki kwa kumfanyia mchezo mmoja.

Walikuwa wakimuonyesha sarafu mbili, moja ikiwa na thamani ya mara kumi zaidi ya nyingine yaani shilingi 50 kwa shilingi 500, na Nasoro siku zote uchagua kuchukua ile ndogo zaidi.

Stori hii ya Nasoro ilizunguka karibia mji mzima.

Siku baada ya siku, vikundi vya wanaume na wanawake vingemwonyesha sarafu hizo mbili, na Nasoro angechagua sarafu ndogo kila wakati.

Siku moja, Mzee Iddi aliyechoka kuona Nasoro akidhihakiwa kwa mtindo huu kila siku, akamuita pembeni ya soko na kumuambia.

"Wakikupa hizo sarafu mbili, chagua ile kubwa zaidi. Ukifanya hivyo utapata hesa zaidi na watu hawatakuona tena kama mjinga."

Nasoro alimjibu, "Ni ushauri mzuri, lakini unajua kama nikichagua kubwa watu wataacha kunipa hela, kwa sababu wanapenda kuamini kuwa mimi ni mjinga zaidi yao."

"Hujui pesa ngapi nimepata kwa kutumia njia hii. Hakuna ubaya wowote kuonekana mjinga au mpumbavu, ikiwa wewe ni mwerevu sana."

โ€ข Mwisho ๐Ÿ˜Ž๐Ÿงต
 

Attachments

  • 20240825_210249.jpg
    20240825_210249.jpg
    1.1 MB · Views: 5
Back
Top Bottom