Story Isiyojulikana ya “Roger Bannister” Alivyovunja REKODI Ya Dunia!..

Story Isiyojulikana ya “Roger Bannister” Alivyovunja REKODI Ya Dunia!..

Seif Mselem

Senior Member
Joined
Oct 16, 2023
Posts
161
Reaction score
526
…kabla ya Mwaka 1954 Dunia ilikuwa…

Haijawahi kushuhudia kwa Muda mrefu Mtu akivunja…

“REKODI Ya Dunia”

…ya Kukimbia RIADHA ya Umbali wa… “MILE Moja kwa DKK 4”

The 4-Minute Mile Record!

Yaan…

Kukimbia umbali wa Kilomita 1.6 Ndani ya Dakika 4 Tu!

Na…

Ilikuwa imepita Miaka 12 tangu Mswedishi…

“Gunder Hagg”

Aweke Record hiyo…

Kwa kukimbia Umbali huo kwa Dakika… 4.06.2

Na…

Kwa muda Mrefu watu walikuwa Hawaamini kama Inawezekana mtu Kikimbia umbali huo kwa Muda mchache Kiasi hicho…

LAKINI…

Ilipofika May 6, mwaka 1954 Mwingereza mmoja Anayejulikana kama…

“Roger Bannister”

Alifanikiwa kuvunja Record hiyo na kuwa Ndio mtu wa kwanza Kukimbia umbaliwa wa Mile 1 Ndani ya DKK 4 Kamili…

Na…

Cha kushangaza Zaidi ni Kwamba…

Baada ya Siku 46 Tangu aweke Record yake MPYA… Alitokea tena Mtu mwingine na Kuvunja Record aliyokuwa anaishikilia Roger…

Yaani… Record ya Roger ilidumu kwa Siku 46 Tu!

Unajua ni Kwanini Haikukaa Muda Mrefu?..

Okay… Subiri baada ya Sekunde 7 Naenda kukwambia ni Kwanini…

Kwahiyo…

Baada ya Roger kuweka Record hiyo na Kuvunjwa ndani ya Siku 46 Tu…hadi Sasa ninapoandika kuna Zaidi ya watu 1700 waliofanikiwa Kuvunja Record hiyo ambayo mwanzo Ilionekana ni Ngumu Kuifikia…

Na…hiyo Record kwa sasa Imekuwa ya KAWAIDA kwa Wakimbiaji Kuifikia!

Nini MORAL Lesson ya Story ya Roger?...

Ukweli ni Kwamba…

Kwenye hii Dunia kitu Chochote kitakuwa KIGUMU tu kama hakuna Mtu amewahi Kukifanya…

ILA…

Ikitokea mtu mwingine Kaweza kukifanya basi hata Wewe unaweza Kukifanya…na Hiyo ndio sababu Kwanini…

Record ya Roger ilidumu kwa Siku 46 Tu ni…

Kwasababu…baada ya Wakimbiaji wengine kuona Roger kafanya basi na wao wakawa na “BELIEF” kwamba wanaweza Kufanya…

Kwahiyo…

Hata wewe unaweza Ukawa unaogopa Kuanza kufanya kitu Flani kwasababu…unahisi Labda hutaweza kukifanya…

ILA…

Ukweli ni Kwamba…kama kuna Mtu yuko mbele yako ameweza Kukifanya hicho Kitu basi hata wewe Unaweza kukifanya…

Sisi wote ni Binadamu, Tunaongozwa na Hisia, Tuna Masaa 24 kwa Siku…

Kama mtu hapa X kaweza kufanya Kitu flani basi na wewe Unaweza…

Njia Rahisi na ya Mkato ni…kumtafuta Mtu anayefanya kitu kama chako then Akufundishe…

Au…

Kwa Lugha Laini Tunasema…

“MODEL” Kile anachokifanya Mtu aliyekutangilia kwenye kile Unachotaka kukifanya…

Hakuna mtu alizaliwa Anajua mambo yote haya…wote Tumejifunza kutoka kwa Watu tunao Waamini…

Na Kama…

Shishi Food anafanya Vizuri kwenye Biashara ya Chakula basi hata wewe Unaweza Kujifunza…

Kama…

Elibarik Alute ana make some Cash kupitia Video Shooting na Photography basi na wewe Unaweza…

Kama…

Ally anatengeneza Career yake kupitia Blogging basi hata wewe Unaweza pia…

Yaani…wao Kuweza kufanya hicho Kitu na wakapata Matunda basi hata wewe Unaweza…

Hiyo Kitaalamu Inaitwa…

“Proof of Concept”

Wao ni kama Roger wamekuwa wa Kwanza na wewe Unaweza kuwa kama wao…

Kuna dalili Nzuri sana unapoona Unataka kufanya kitu na Tayari kuna watu mbele yako wanakifanya na Kufanyikiwa nacho…

Tofauti na hapo Ukiamua kufanya kitu cha Pekee yako hakiksha umefanya “MARKET Analysis” Vizuri + una Experience na unachokifanya ili ujue Trend ya Market inaendaje…

Vinginevyo…utakuwa kama Rafiki zangu wa FX uta Burn Bank Account yako…

So kwa ku Summarize Tu ni kwamba…

Kama kuna Mtu anafanya Kitu kama unachofikiria kukifanya basi hiyo ni Ishara nzuri ya wewe kufika Alipo…

Kwasababu utajenga… “IMANI”

Belief + Despline = Sucesss

Vile vile…

Mtafute mtu unayemuamini kwenye kile Unachofanya kisha Mfanye awe Mentor wako…

Jifunze na Fuatilia kila Kitu kuhusu yeye…

Usimpe kila mtu Airtime kwenye Kichwa chako utachanganywa…

The WORLD Is too Complex… You can NOT Master Everything!

Tafuta watu wako wa 5 Unaowaamini na Wanaoendana na kile Unachotaka Kufanya then wafanye kuwa Mentors zako na Kisha tega Sikio kwao.

Sio kila Mtu wa Kumsikiliza.

Uwe na Siku Njema!

Gracias…[emoji1317]

Omeona Sasa hadi Nataka Kusahau…

By the way...

Kama Umependa Makala hii basi Utaipenda Zaidi inayokuja...

Kwahiyo Ili Usipitwe...

Usiache ku Like na ku Comment Chochote hapo Chini au kama Una swali Pia Unaweza Kuuliza (Nitajibu Mimi Mwenyewe)!

Seif Mselem
rogerbannisterposter-1446235202.jpg
 
Back
Top Bottom