MWANDISHI: INVYOLATA SHIRIMA(Neema)
Kulikuwa na kijiji kimoja kilichojulikana kama same.
Na ndani ya hicho kijiji kulikuwa na Mzee mmoja aliyejulikana kwa jina lake MzeeOtonglo.
Kabla Mzee huyu alikuwa akiishi katika kijiji cha kijichi ambapo huku ndipo alipokulia. Na baadae aliweza kumilikishwa kipande cha ardhi na wazazi wake ikiwa ni huko same. Baada ya wazazi wake kupendezwa na tabia yake Kwani alikuwa mtiivu na msikivu juu yao.
Na huku ndipo Mzee Otonglo alipoenda kuanzisha maisha yake yeye pamoja na familia yake baada ya kuoa. Na alibahatika kupata watoto watoto wakiume na wakike.
Bobu akiwa ni mtoto wapili(2) kuzaliwa katika familia ya MzeeOtonglo akitanguliwa na kaka yake ambaye ndiye mkubwa na kufwatiwa na wadogo zao watatu(3).
************************
Wakati wote huko shuleni Bobu alionekana kuwa na jitihada sana katika masomo yake. Jambo lililompelekea ufaulu katika mitihani yake ya mwisho ya darasa la saba. Lakini kutokana na hali ya uchumi katika familia yao haikuwa nzuri alishindwa kuendelea na elimu yake zaidi na kuishilia kuwa nyumbani.
Bobu alianza kuyaishi maisha rasmi ya mtaani bado katika umri mdogo. Aliweza kujikita katika vibarua mbalimbali yote ili aweze kujipatia shilingi na kujikwamua kuondokana na umaskini.
Na kuwa kawaida yake mara nyingi kuzunguka katika baadhi ya maofisi kujaribu kuomba vibarua. Na hatimaye alifanikiwa kupata kibarua cha kudumu katika ofisi mojawapo pale kijijini.
Wakati bado akiendelea na kibarua chake hicho aliweza kupata ushawishi na kutaka kujiunga na kikosi fulani ndani ya nchi yake ili aweze kuitumikia. Ambapo alishawishika kutokana na mafunzo yake. Hata hivyo alifanikiwa kujiunga katika kikosi hicho kwa miaka kadhaa akipata mafunzo na baadae alihitimu na kubahatika kupata ajira ndani ya kikosi hicho ikiwa ni ndoto yake ya muda mrefu.
Siku moja kwa rafiki yake na Bobu ambapo ni jirani na kwao kulikuwa na shughuli hivyo walialikwa watu kadha wa kadha kwenye shughuli hiyo bila kujali rika. Bobu naye akiwa ni miongoni mwa walioalikwa kuhudhuria kwenye shughuli hiyo.
Hakukosa kufika kwenye shughuli hiyo na wakati shughuli hiyo ikiwa inaendelea. Bobu aliweza kupata muda mzuri akawa anapepesa macho yake huku na huko. ambapo katika ziara yake yote mboni zake za macho ziliweza kutua kwa binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Sikudhani. Bobu alivutiwa naye nakujikuta akiendelea kumtizama mara nyingi jambo ambalo hata sikudhani yeye mwenyewe aliligundua na akawa anajiuliza maswali mengi kichwani bila majibu.
Wakati shughuli ikiwa bado inaendelea Bobu alionekana kunyanyuka pale alipokuwa ameketi nakuelekeza hatua zake mpaka ulipokuwa mlango na kutoka nje. Na muda kidogo alirejea alipokuwa. Ambapo shughuli hiyo ilipokuwa inakaribia ukingoni Bobu aliweza kuondoka katika eneo lile moja kwa moja wala hakuweza kuonekana tena.
Na baada ya shughuli hiyo kutamatika watu walianza kutawanyika kurudi kwao. Sikudhani naye pia alianza safari kwaajili ya kurudi kwao.
Mara tu baada ya hatua chache alizopiga sikudhani mbele kidogo aliweza kufunikwa bushuti kuanzia kichwani na kushuka nae mpaka chini miguuni na mtu ambaye hakuweza kumwona wala kumfahamu.
jambo ambalo lilimtia wasiwasi mwingi wakati akiendelea kujisaidia ili aweze kutoa lile bushuti alitahamaki kubebwa na kuwekwa begani kama vile vibega wabebavyo mizigo Sikudhani alijaribu kujitetea kwa kila namna aliyoweza lakini alishindwa.
Baada ya hatua kadhaa kutoka pale yule mtu alifika mpaka alipokuwa amekusudia akamketisha Sikudhani katika kiti na kisha kumwondolea lile bushuti.
Ambapo Sikudhani aliweza kuona kutokana na mwanga hafifu uliokuwa ukiangaza pale. Na wakati akiendelea kushangaa mazingira yale macho yake akiyapepesa kila pande pembeni yake alibahatika kumwona mtu. Na alipojaribu kumtizama kwa umakini zaidi Sikudhani aliweza kuikumbuka sura yake vizuri na hakuwa mwingine bali alikuwa ni Bobu ambaye aliweza kumwona katika shughuli ile.
Sikudhani hakupendezwa kuendelea kuwa pale kwani muda ulikuwa umeenda sana kiasi cha kwamba muda huo alitakiwa awe yupo nyumbani. Hata hivyo alihamua kumuuliza Bobu ili ajue chanzo cha yeye kuwa pale "ni nini haswaa?!"
Akioneka kuwa na hasira sana. lakini hakuweza kupata jibu lolote kutoka kwa Bobu zaidi ya ukimya na ukimya huo uliendelea kutawala mpaka palivyopambazuka asubuhi. Kwa wakati huo wote maswali yalikuwa ni mengi yaliyorindima katika akili ya binti Sikudhani asijue lipi lakufanya zaidi aliruhusu hukumu ya lawama juu yake baada ya yeye kushindwa kutoroka mikononi mwa Bobu.
Hivyo ilibidi taratibu zote zifwatwe kwa mila na desturi kama ilivyohitajika. Kwani ni kawaida katika jamii nyingi za afrika pale binti anapoolewa nilazima haya yatendeke kama hatua za awali kabla ya ndoa.
Baada ya hayo lilifwatia zoezi zima la ndoa ili kuwaidhinisha kama Mume na Mke halali.
Bobu na Sikudhani waliweza kufanikisha zoezi hilo pamoja nakuanza maisha yao mapya wakiwa ni wanandoa tayari. Na muda mchache tu mara baada ya ndoa Bobu alichaguliwa kuwa balozi na wanakijiji katika mtaa wao. Wengi wao wakiamini anaweza kutokana na kazi yake aliyokuwa nayo. Kazini nako alihamishwa katika kitengo chake alichozoeleka kufanya kazi na kuhamia katika kitengo kingine cha juu yake.
Mabadiliko yalianza kujitokeza kwa bobu siku hadi siku na kujikuta akionyesha makucha yake hadharani bila kujali. Hata utu aliokuwa nao ulipotea na kugeuka kuwa mtu katili na korofi asiyeambiwa kwa chochote tofauti na alivyokuwa akitazamiwa.
balaa lisiloisha huko nyumbani mkewe alikuwa akipokea vipigo vya mara kwa mara sababu zikiwa ni nyingi ambazo hazikueleweka. Mojawapo kati ya hizo ikiwa alichelewa kupata mtoto na ni miaka kadhaa imepita toka ndoa yao.
Hata hivyo licha ya changamoto zote hizo lakini Sikudhani pamoja na Bobu walibarikiwa kupata mtoto wakike na wakamwiita Majaliwa. Hapo kidogo amani ilirejea ndani ya nyumba ikiwa ni baada ya Bobu kujirudi na kupunguza ukatili aliokuwa akifanya. Hata hivyo amani hiyo iliweza kutoweka tena ndani ya muda mfupi.
Kutokana na kitendo cha Bobu kuwa na wanawake wengine huko nje na hivyo amani hiyo kushindwa kudumu muda mrefu. Hivyo mateso yaliendelea kama awali na yalizidi baada ya kushindwa kupata tena mtoto.
Sikudhani hakuridhia tabia hiyo ya mumewe alihamua kufanya uchunguzi na aliweza kugundua baadhi ya wanawake waliokuwa michepuko ya mumewe. Jambo ambalo lilimuuma sana baada ya kumgundua hata na rafiki yake wa karibu aliyekuwa akimwamini naye alikuwa ni miongoni mwa hao waliomkosesha amani katika ndoa yake. Wakati naye alikuwa na ndoa yake tena yenye amani kwani Mume wake alionekana ni mtu aliyetulia asiye na mahangaiko kama ilivyo kwa mkewe.
Baada ya kugundua yote hayo sikudhani alikosa uvumilivu na kuhamua kuondoka kurudi kwa wazazi wake. ambapo aliweza kukaa huko kwa muda mrefu mpaka mumewe alipomfwata na kumtaka arudi.
Hivyo Sikudhani aliweza kurudi kuendelea na maisha yake ya ndoa. Lakini Bobu mara hii alionekana kuwa mnyonge sana kuliko ilivyokuwa kawaida yake. Ikionekana kuna jambo ambalo alimficha mkewe na hakutaka ajue. Hata hivyo mkewe hakuweza kutambua chochote zaidi alihisi mumewe amehamua kubadilika na kujirudi.
Lakini kadri siku zilivyozidi kusonga hali ya Bobu ilizidi kubadilika akawa ni mtu wa homa mara kwa mara jambo lililoanza kumtia wasi wasi Sikudhani kutokana na hali ya mumewe. Na baada ya vipimo waliweza kugundulika kuwa na maambukizi ya (VVU) hivyo walianzishiwa rasmi kupokea matibabu ya dawa.Taarifa hizi zilimshtua sana Sikudhani na kumkosesha uvumilivu hata akajikuta anakata tamaa ya maisha na kuhamua kuchukua maamuzi magumu ya kujinyonga na kumwacha Majaliwa bado mdogo.
Majaliwa aliendelea kulelewa akiwa chini ya uangalizi wa baba yake akisaidiwa na wazazi pande zote mpaka alipomaliza shule kidato cha nne(4). Ambapo hakufanikiwa kuendelea zaidi kutokana na changamoto alizokuwa akipitia kuwa ni nyingi na kumsababishia anguko hilo.
Hata baada yakumaliza shule Majaliwa hakuweza kuondoka pale kijijini kwao kwani baba yake hakumruhusu kuondoka kwenda popote ili kujitafutia maisha ikiwa wenzake wote aliomaliza nao shule walishaondoka. Majaliwa aliendelea kuwa bado pale kijijini ambapo hakuweza kujipatia mahitaji yake baadhi aliyokuwa akihitaji na hii ikawa ni changamoto kwake isiyo na mtatuzi.
Siku kadhaa pale kijijini kwao kuna kijana mmoja aliweza kufika sura yake ikionekana kuwa ng'eni maeneo yale na kwa muonekano kijana huyo alionekana mtanashati. Hata hivyo kijana huyo alionyesha kumpenda Majaliwa lakini Majaliwa kwa wakati huo hakuwa tayari kuwa na mpenzi. Lakini kadri siku zilivyozidi kusogea Majaliwa akajikuta akishawishika na kushindwa kujizuia kumpenda mwanaume huyo ambaye alionekana kuwa msaada kwake kutokana changamoto alizokuwa akipitia wakati ule.
Ambapo walihamua kufanya mahusiano hayo kwa siri sana ili baba yake asiweze kutambua chochote kilichokuwa kikiendelea baina yao.
Ikiwa ni muda umepita Majaliwa alianza kujihisi utofauti katika mwili wake na alipoenda kupima aliweza kujigundua kuwa na ujauzito. Na taarifa hizo zilipomfikia mwanaume huyo aliyehusika na ujauzito huo aliweza kumkatalia.
Nyumbani nako alifukuzwa baada ya kugundulika kuwa na ujauzito akimshutumiwa kuleta haibu. Majaliwa hakuwa na jinsi aliweza kuondoka na kwenda kuishi kwa bibi yake. Licha ya maisha kuzidi kuwa magumu kule Lakini alifanikiwa kujifungua mtoto wake salama na kuanza kujishughulisha na biashara ikiwa ni kuuza mboga. Ili aweze kuyamudu maisha yake pamoja na mtoto kwa wakati bado akiwa pale kwa bibi bila kumsumbua.
Bobu ambaye ni baba mzazi wa Majaliwa alifariki dunia kutokana na maradhi yake. Ambapo aliweza kuacha watoto kadhaa na hii ikijidhihirisha wazi kuwa Bobu alikuwa bado hajatulia hata baada ya kifo cha mkewe.
Na baada ya kumalizika kwa msiba wake ndugu zake walianza varangati kupigania mali za marehemu bila kujali familia aliyoiacha. Ambapo hakuna mtoto wa marehemu hata mmoja aliyemilikishwa moja ya mali zake. Majaliwa naye akiwa ni miongoni mwao waliambulia tupu hakuna aliyejali kuhusu wao.
Majaliwa aliendelea na biashara yake kama hapo mwanzo na katika pilika pilika zake za hapa na pale alibahatika kukutana na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina kama Bahati. Ambapo walifanikiwa kuunga urafiki kutokana na biashara yake. Ambapo urafiki huo ulidumu na kuzidi kuimarika siku hadi siku hata wakaridhiana na mwisho wa siku wakahamua kuoana.
Ambapo baadhi ya ndugu zake na marehemu ikiwa ni baba zake wakubwa kwa wadogo walipopata taarifa hizo waliweza kujitokeza na kudai mahari jambo ambalo halikufanikiwa.
Maisha ya Majaliwa yalibadilika ghafla na kuachana na ile biashara yake aliyokuwa akiifanya baada ya kukabidhiwa biashara mojawapo na mumewe ili kuisimamia.

Upvote
0