Story ya chips egg far far or confuse

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna Mzungu alikuja Tanzania kwa shughuli za kikazi. Katika mihangaiko yake alisikia njaa na muda wa lunch uliwadia. Alifikiria pa kupata chakula, aliamua kutafuta sehemu inayouza chakula apate rizki.

Alikuta kijiwe cha chips na wasela kibao wanapata msomi. Alikaribia ile sehemu, kulikua na foleni ya kutoa order, ukisha toa order unakaa na kuketewa kinywaji kama kimo katika order yako.

Mwenye biashara kumuona Mzungu hakutaka hata kuinua uso macho yao yagongane. Aliangakia wateja wa nyuma ya mzungu na kuchukua order zao. Kuna dogo muosha vyombo alimuona Mzungu amesimama muda mrefu pale. Alijua boss wake lugha imemshinda.

Dogo alifika kwa mzungu akamuuliza Do you want chips egg? Mzungu akajibu yes, dogo akuliza chips egg far far or confuse, Mzungu alishaona order nyingi pale ni zege. Alijibu confuse, dogo aliendelea mirinda coke fanta?

Yule Mzungu aliusifu sana ujasiri wa dogo uliofanikisha mauzo.

 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nakumbuka hiyo siku. Mimi ndio nilikuwa mmenya viazi. Siku hazigandi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…