Story ya Philibert Kabago

Story ya Philibert Kabago

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
Inaendelea...

Kundi la Boy with Voice liliendelea harakati zake hadi ilipofika mwaka member wa kundi hili " Hamad saleh alipotangulia mbele za Haki, ilikuwa tarehe 12 /12/2010.. kwa hivyo Baada ya msanii Hamad kutangulia mbele za haki , na hapo nyuma wakati yupo hai tulikuwa tunafanya nyimbo nyingi sana na yenye, jina lakabaki la kundi " Boys with voice" ila mimi kama Philibert kabago ndio nilianza Rasmi kufanya kazi zangu nje ya kundi nikiwa kama solo Arts..

Kuna kazi ambazo nilifanya kama vile

1. Project / nyimbo ya moyo wangu nikiwa na msanii Mb doggy kipindi ndio producer Q the done bado mgeni ndio anafika mwanza Tena nakumbuka na ngoma hii nilifanya mwaka 2007,

2. Lakini pia ngoma nyingine inaitwa " Samahani Dear" hapa nilimshirikisha chelea man na mwana Dada keisha kutoka Crew ya Tip top Conection.

3. Na ngoma nyingine pia inaitwa " nina mwingine ambapo humu pia niliwashirikisha wasanii wawili msanii Chelea man na P.n.c hizi mbili tulifanyia katika studio za " Tetemsha production"

Baada ya hapo nikaendelea na kazi yangu ya " Utangazaji" Baada ya Rafiki yangu Hamad kuwa amekufa hiyo 2010. Nikaamua pia ninaweza kuiendeleza " Boys with Voice" huku mimi nikiwa nafanya kazi zangu nje ya kundi nikiwa kama solo Artist,

Kwa hiyo ukiachana na hizo project nilifanya mwaka 2007 pia zipo zingine pia nilifanya nje ya kundi nikiwa kama solo Artist. Ndio mwaka 2010 ndio nakatoa project kadhaa kama

1. Hakuna kuremba
2. Umeme wa mgao
3. Nenda salama nimefanya na mdogo wangu Anaitwa Gozbert , baada ya mama yetu mzazi kufariki

Nilitoa pia Album iliyojulikana kwa jina la " Moyo wangu" ambayo kiukweli ilifanya Vizuri sokoni, kipindi ambacho kuingiza Album sokoni ilikuwa inahitaji maarifa na juhudi kubwa sana kwa wasanii,

Kwanza Uwe na hit song katika Album yako ili uweze angalau kuwashawishi wahindi " wadosi" waweze kuinunua Album yako , kwa maana Enzi hizo wao ndio walikuwa wanunuzi wa kazi za wasanii na wasambazaji pia sokoni .

Kiukweli niliweza kuwashawishi hadi ikapelekea wakazarisha Album yangu kwa wingi Sokoni katika mifumo miwili (2) tofauti , katika mfumo wa kawaida wa cassette na mfumo ambao kwa kipindi hicho ndio kwanza ulikuwa unaingia ( mfumo wa Cd ) .. kwahiyo mashabiki zangu walipata fursa ya kununua Album yangu kwa wingi sana, Hasa wale ambao walikuwa wamenunua Radio kubwa Enzi hizo ambazo zilikuwa zina Support mfumo wa Cd.

Kiukweli nilimshukuru Mungu baada ya kuonana mapokeo ya Album yangu yamekuwa makubwa ilipoingia sokoni..

Lakini pia kuna baadhi ya kazi zangu pia hazikubahatika kutoka baada ya mimi kufocus na inshu ya Utangazaji nyimbo kama vile.

1. Ray ni ngoma ambayo nilifanya mimi na msanii sajina
2. Tanzania wimbo ambao nilifanya na msanii anaitwa " Hard mad"
3. Na wimbo unaitwa" kabago " ambao ulikuwa na ujumbe unaohusu maisha yangu kwa ujumla na Support yangu pia kwa wasanii wa hapa jijini Mwanza.

Mpaka sasa nafikiria kutoa Album ama Ep iliniweze kusijumulisha ndani yake, Kwa sababu pia nimetoa Support kwa wasanii wa hapa hapa jijini mwanza lakini pia hata kwa wasanii ambao wanaishi nje ya Mwanza ambao kwa sasa wamekwisha kuwa mastaa wakubwa sana katika Tasnia hii ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Lakini pia niliweza kufungua Studio inaitwa " kili Record" Studio ambayo Producer alikuwa ni mdogo wangu anaitwa Gozbert jina maarufu alijulikana kama " loli mwaa ama "loli pop"

Alitoa ngoma kibao na kali kama vile.

1. Basi nenda ya MO music
2. Nahitaji maadui wimbo wa Dogo D akiwa na Rapper young Killer

Nilifanya hivi kuanzia kuwapa support nikiwa kama Radio prisenter katika kituo cha Radio kwa kucheza kazi za wasanii hao lakini pia kufungua hiyo Studio ya kili Record na kuwapa furaa ya kurekodi nyimbo kwa gharama ndogo na hata muda mwingine Bure.

Itaendelea..

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 

Attachments

  • images-28.jpg
    images-28.jpg
    33 KB · Views: 9
Back
Top Bottom