Hakuna mchezaji asiyevuta bangi
Ni kama wasanii wanapokua studio.
Kabla ya kuingia booth kuingiza vocal, wasanii wengi(kama sio wote) huwa wanavuta bangi kidogo ili kuweka kichwa sawa, na pia bangi huwa ni kama inazibua masikio.(kama huamini jaribu, halafu nenda kasikilize mziki)
Ukivuta bange masikio huzibuka dizain
fulani(ukisikilza wimbo unauskia katika kila angle, mpangilio wa sauti zooote unaziskia peke yake, beat lote unalisikia peke yake, hata kama kuna nini unakisikia vizuuuri peke yake).
Haya nayasema kwa sababu nimezunguuka sana kwenye studio, wasanii wote wakubwa kwa wadogo ni lazima wavute bangi, hata waimba kwaya wanavuta.
Kuna msanii mmoja mkubwa sana alikujaga studio akawa ni kama anaona aibu wakati wa kuingiza vocal, akapewa bange astue, baada ya hapo ngoma aliyorekodi ilikua hit.
Angalia ngoma ya mbosso shilingi yang'ara ng'ara angalia jicho la mbosso, mchizi hiyo video alivuta bange ile mbaya, jicho jekunduuuuuu.
P funk alimpiga afande sele bonge moja la kofi pale bongo record sababu ya kuvuta bange.
Kuna studio ukiingia, mtu alieko umbali wa mita moja huwezi kumuona, mimoshi mwanzo mwisho chumba kizima.