Angalia tena postings zangu; sikusema kuwa twende tukopi Azimio la Arusha la 1967 kama homoemorphism, yaani one to one mapping kama lilivyo. Nilikubaliana na Steve kuwa kuna haja ya kurudia Azimio lile na kuondoa mapungufu yake. Mapungufu makubwa katika Azimio lile yalikuwa ni yale ya kuendesha uchumi wa nchi nzima kijamaa na hivyo kuua moyo wa ubunifu wa watu. Lakini mambo mengine kama vile investment katika watu kwa kupambana na maadui wa ujinga magonjwa na dhuluma yanatakiwa yarudishwa. Vile vile tunatakiwa kujenga uongozi wa wazi unaowajibiki kwa nchi ikiwa ni pamoja kuimarisha utawala wa kisheria, kujenda demokrasi thabiti ambamo mipango ya nchi inapangwa kwa uwazi ikiangalia maslahi ya nchi, na hivyo kuondokana na rushwa kama hizi za Richmond.
Nimeshasema kuwa tatizo lilikuwa kwenye Ujamaa. Nadhani umeelewa.
Pamoja na ubaya wa ujamaa, napenda kukumbusha kuwa ukuaji wa deni la nje la Tanzania ulianza haraka sana baada ya Nyerere kuondoka madarakani. Mara tu baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha na kutaifisha mali za binafsi (ambayo kweli ilikuwa ni kosa kubwa sana) Tanzania haikupata mikopo sana kutoka nchi za nje; kukosekana kwa mikopo hiyo ndiko kulikopelekea nchi kushindwa kujiendesha mara baada ya vita, na hasa baada ya Nyerere kukataa masharti ya IMF. Tanzania ilianza kupata mikopo tena wakati wa Mwinyi baada ya kufikia makubaliano na IMF.
Microsoft Windows Operating System ilianza kama Microsoft DOS mwaka 1984. Baadaye ikafanyiwa ukarabati na kuwa MS DOS 2.0, ikaendelea na kufanyiwa ukarabati kidogo kidogo kwa kuondoa mapungufu yaliyoonekana na kuongeza features mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90 ikabadilika kuwa MS Windows ambayo nayo iliendelea mkiufanyiwa ukarabati mpka leo hii tuna Windows Vista. Recycling kwa kuondoa mabaya na kuongeza mazuri ni sehemu ya ubunifu. Magari yote unayoendesha leo hii ni matokeo ya kurecycle Quadracycle ya Ford ya mwaka 1896.
Kichuguu:
IMF mara nyingi sio chombo cha mikopo. Chombo cha mikopo ni World Bank. IMF wanachoangalia ni Miundo ya uchumi wa nchi na nini nifanyike.
Tanzania ilikopeshwa sana na World Bank kabla ya uchumi wetu kuanguka kabisa. Kasome sera za Robert MacNarama, aliyekuwa rais wa Benki ya dunia kati ya 1968 mpaka 1981. Jamaa huyu alitoa mikopo mingi kwa nchi za dunia ya Tatu hili kuongeza huduma za jamii. Na alikuwa anasema Benki ya dunia ikiweza kusomesha watu na kutoa huduma za afya basi nchi za dunia ya tatu zinaweza kuendelea. Lakini wakati anaondoka madarakani nchi zote alizokopesha zilikuwa kwenye madeni makubwa ikiwemo Tanzania. Hizi data zipo, jaribu ku-google zitakuja tu.
Kuna critics wa namna mbili wa Robert MacNarama. Wale wa upande wa kulia wanasema kuwa Benki ya dunia ingeshugulikia kazi zake za kibenki kama ilivyo miaka ya nyuma na kuachana na kutoa huduma za jamii. Kumbuka kabla Robert MacNarama ajakuwa rais wa benki ya dunia, benki hiyo ilikuwa inamkatalia kumpa mikopo kwa sababu ya sera zake.
Critics wa upande wa kushoto wanasema Robert MacNarama alikuwa ni waziri wa ulinzi wa Marekani. Na aliacha kazi hiyo na kuwa rais wa benki ya dunia hili kupambana na nchi za kijamaa kwa kutumia mikopo. Hivyo Marekani haikuwa na haja ya kupambana kijeshi na Ujamaa wa Kitanzania na walitumia mikopo.
Kwa vyovyote vile watanzania mlikuwa naive na mikopo na ikatumika vizuri ku-prove kuwa ujamaa ulikuwa ni wrong.
Kuhusu MS-DOS. Kuna tofauti kubwa sana. Kwa wewe mtumiaji unayepewa look and feel unaona DOS iliendelea mpaka kufikia Vista. Lakini architecture ni tofauti sana.
Vilevile kuhusu magari naona umechukua mfano kutoka kwenye kile kitabu cha Nyerere cha hotuba zake za UJAMAA. Na hapo babu kifimbo alikuwa wrong. Ford hakufanya invention ya magari. Kabla ya 1896 Magari yalikuwa yanatembelea duniani. Alichofanya Ford katika utengenezaji wa magari ni kutumia falsafa ya Adam Smith. Adam Smith alisema kuwa uzalishaji unaongezeka kwa watu ku-specialize na kufanya kitu kimoja. Ukiwa na kiwanda cha viatu, basi mtu mmoja kazi yake iwe kutengeza soli, mwingine kushona ngozi, mwingine kukata ngozi na mwingine kuunganisha vitu vyote. Lakini ikiwa mtu mmoja anatengeza viatu kuanza mwanzo mpaka mwisho basi uzalishaji unakuwa mdogo.
Kwa mtaji wa Adam Smith, Ford alichofanya ni kuanzisha assembly line katika utengenezaji wa magari. Kina mfanyakazi alikuwa na kazi moja tu na mtindo huu ulizidisha uzalishaji wa magari na kupunguza bei.
Ujamaa na Azimio la Arusha ni kitu kimoja. Ujamaa ilikuwa ni nadharia na Azimio la Arusha implementation.