Stress ni nini?

mbwana semsimbazi

Senior Member
Joined
Sep 5, 2013
Posts
196
Reaction score
202
STRESS NI NINI..?

1. Je stress ni pale unapompa msichana lift halafu akazimia ndani ya gari yako na humjui wala hujui kwao. Ulimkuta tu njiani ukamsaidia.!

2. Au stress ni pale unapoamua kumpeleka huyo msichana hospitali na akabainika ana mimba dokta akaanza kukupongeza kuwa unakaribia kuitwa baba!

3. Labda stress ni pale unapokataa na kumwambia dokta mimba si ya kwako, mara ghafla msichana anazinduka na kudai mimba ni ya kwako?

4. Huenda stress ni pale dokta anapoamua kukupima ili kuthibitisha, na baada ya vipimo anakwambia mimba si yako kwakuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba.!

5. Au stress ni pale
unaporidhika majibu ya doctor kuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini unakumbuka nyumbani una mke na watoto wawili.??

JE STRESS NI NIN!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…