rikiboy
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 21,952
- 43,265
Hakuna kipindi kigumu kama Kumaliza Chuo alafu ukiwa na expectations kubwa za Kupata ajira na maisha mazuri then Siku zinasonga hata dalili ya kupata ajira hakuna, CV umetandaza karibu ofisi zote mjini lakini hata kuitwa kwenye Interview hakuna hapa ndo muda Vijana wengi hujihisi useless na hutamani kufanya chochote wafanikiwe.
Sio ajabu kwenye Mabanda ya Kubet wamejaa vijana wa Vyuo ambao wanaamini kupitia kubet watatoboa maana kujiajiri kwa biashara zinazohitaji mtaji mdogo wengi huona ni Kujidhalilisha, start from scratch sio kitu rahisi na wengine hufail hapo ndo mwanzo wa kuanza kujiunga na Makundi mabaya ya Uvutaji bangi hata Uhalifu.
Nilipomaliza chuo nilikaa miezi sita bila ajira hakika nilijichokaa nikaamua kuweka Degree pembeni nikaanza Kuuza mitumba jambo ambalo mwanzo nilishindwa kulifanya sababu ni
1. Mazingira ya nyumbani hakika ingekuwa ngumu zaidi kuungana na vijana niliowaacha mtaani waliamini nimesoma hivyo kufanikiwa ni rahisi leo hii Nipo nao Tunauza mitumba.
2. Ningesema niende mbali na nyumbani ambako hakuna anaenijua ingekuwa at least lakini ningeishi vipi maana hata ndugu nao wanakuchoka wachache sana tena labda ndugu wa damu wanaweza kukubeba bila maneno na masimango.
Lakini hayo yote yalipita nikajitahidi kuzoea maneno na vidole vya watu sababu its my Life kiukweli nikaanza kupata mia mia ambazo zilinisaidia kupunguza stress za Kuajiriwa na kukaa tu bila cha kufanya. Lakini pia Nikaanza kujifunza kuendesha boda boda na bajaji ili at least nipate mtu atakaeweza kunipa chombo chake nimfanyie kazi. Nilipofanikiwa kupata leseni nikaacha kuuza mitumba nikaanza kuendesha bodaboda siku zikaenda maisha yakasonga siku isiyokuwa na jina nilipigiwa simu nahitajila kwenye Interview pale nilipopeleka CV yangu mtu mwenye position kama yangu ameacha kazi hapo ndio ukawa mwanzo mpya wa maisha ya kuajiriwa.
Nikagundua Why Graduate fail in really life??
1. Wengi huweka expectations kubwa zaidi kuliko hali halisi
2. Wengi hawataki kulower their standard sababu ya kuogopa macho na maneno ya jamii inayomzunguka
3. Hawana watu wakawapa mawazo positive na ushauri nini cha kufanya zaidi ya kuambiwa ajira ni ngumu siku hizi
4. Wengi hutumia muda mwingi kujuta juu ya muda waliopoteza wakiwa chuo kusomea course ambayo leo hata ajira ya kujitolea anakosa.
Hustle gani ulipitia baada ya Kumaliza Chuo??? Je ulifanikiwa kupata ajira??