Stress za maisha hazisababishi vidonda vya tumbo

Stress za maisha hazisababishi vidonda vya tumbo

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kumekuwa na imani kuwa vidonda vya tumbo husababishwa kwa kiasi fulani na stress za maisha na msongo wa mawazo . Hili jambo si kweli.

Stress zinazosababisha vidonda vya tumbo ni pyhsiological stress, hii ni stress inayotokea pale mwili unaposhindwa kufanya kazi vizuri. Mara nyingi hii hutokea kwa wagonjwa mahututi.

Asilimia kubwa ya vidonda vya tumbo husababishwa na bacteri wa H. Pylori. Hawa huambukizwa kwa kula vyakula vichafu(vilivyochanganywa na kinyesi).

Asilimia 90 ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo hupata kwa njia hii. Na hivi vipo sana mjini sababu tunakula sana kachumbari zilizotengenezwa na watu waliochambia mikono na kushindwa kunawa vizuri au kujisanitize.
 
Watu wengi wanatembea na huyo bacteria
emoji3083.png
ila kitu kinachompa nafasi huyo bacteria wakati wa stress ni mtu kutokula vizuri na hivyo bacteria anapata nafasi ya kushambulia
 
Watu wengi wanatembea na huyo bacteria [emoji3083] ila kitu kinachompa nafasi huyo bacteria wakati wa stress ni mtu kutokula vizuri na hivyo bacteria anapata nafasi ya kushambulia
Ni kweli wengi wanatembea navyo lakini kutokula hakumfanyi ashambulie zaidi bali kutokula hufanya maumivu ya vidonda yawe makali zaidi. Sababu ni kuwa chakula kikiwapo tumboni huwa kinapunguza makali ya asidi katika kuchoma vidonda.
 
Mkuu, naomba nichangie hivi....!!

Kisaikolojia mtu apatapo msongo ama stress, huathirika zaidi akili ambayo ni intelligence ambao ni untouchable na akili inatokana na aither uimara au udhaifu wa ubongo ambao ni brain na ni touchable thing. Pale msongo unapozidi kuna aina za hormones zinazozalishwa kwenye magamba yaliyopo kwenye ubongo na kusafiri kupitia oxgen na damu mwilini ikiwemo hadi tumboni.

Sasa kinachotokea ni kuwa mtu mwenye msongo anapozidiwa na aina hizo za hormones zinazoathiri mambo mengi ikiwemo kupoteza hamu ya kula kuharibu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kukata hormones za furaha nk hupelekea sehemu mbalimbali za mwili kuwa under control na hizo hormones na kusababisha matatizo ikiwemo na vidonda vya tumbo.

Hao bacteria unaweza kuwa nao na usiwe na vidonda ila unapopatwa na kushuka kwa ufanisi wa mwili unaotokana either na stress au mengineyo husababisha.

Nimetoa picha ndogo tu lakini ni kweli stress zinachangia.
 
Hapa nimevurugwa, ila najaribu kuelewa, mtoa mada amesema ni physiological stress ndiyo zina sababisha na wewe umegeneralise kuwa ni stress. Hapa napata picha kuwa stress zinaleta vidonda vya tumbo ila physiological stress.
 
Kabisa mkuu
 
Yap na physiological stress ni tofauti na stress inatotokana na mawazo, ugumu wa maisha na matatizo mengine ya maisha. Hii hutokea watu wakiwa wagonjwa sana kama wale wa ICU au wagonjwa wa muda mrefu wa magonjwa makubwa kama figo, ini , kansa nk.

Nahisi watu walivyosikia stress wakafikiri ni hii stress tuliyozoea.
 
Dunia bhana ,ukinunua net ili ujilinde dhidi ya Malaria Cancer inakuchukua, Ukijikinga dhidi ya Ngoma ,Presure au Pneumonia ina wewe, ukijihadhari na Magonjwa yoote Mara basi la kimbinyiko unaanguka nalo unakufa, yaani ni kama vile Dunia inatuchola tu.

Cha Msingi hapa mtumikie tu Muumba wako ili badae usitirike kule uendako.
 
Back
Top Bottom