Strictly kwa wenye familia: Jicho la kupima mafanikio

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
1,667
Reaction score
362
Kipekee niwapongeze kwa kuwa na familia.

Raha ya familia hunifanya niamini kuwa family is a gift from God na sote tuna responsibility ya kuwajibika kuifanya kuwa sehemu ya pekee kwenye mzunguko wetu wa maisha.......Hongera kwa kuwa na familia

Kuna tendency maarufu sana unakuta mtu anakubalika sana kazini kwa kufanya kazi vizuri sana kazini na kujituma, ni mtu ambae anafahamika na kusifika sana kazini uwezo wake wa hali ya juu katika kutatua matatizo ya wengine maofisini mwao. Utakuta labda ni mchungaji anasifika sana kwa kusuluhisha ndoa za wengine, lakini yeye mwenyewe kwake hali kiwa tofauti au utakuta mtu ni manager mzuri ambae wafanyakazi na watu wote ofisini kwake wanampenda na hawangependa wakati wowote asiwepo....Mtu huyuhuyu ukigeuza upande wa pili utagundua kuwa nyumbani mke/mume na watoto wanatamani hata asirudi.

Utakuta mtu anasifika na wafanyakazi wenzake kuwa mtu mwema sana kwa kuwa huwa anawatoa sana lunch wakati wa kazi au kwa marafiki kwa kuwapiga round sana lakini hajawahi hata siku moja kufanya hivyo kwa mkewe au kwa watoto

Naomba tu nitoe ushauri wangu, PIMA MAFANIKIO YA MAISHA YAKO, KAZI YAKO, BIASHARA YAKO etcetera AT THE LENS OF YOUR FAMILY. Kama unafanikiwa sana kwenye shughuli zako lakini na unasifiwa huko kazini au mtaani lakini nyumbani hali ni tofauti just count yourself as a looser.....

Nakutakia mwisho mwema wa week na familia yako....bila shaka utajitahidi kuhakikisha familia yako inaanza kukuona yule mtu mzuri ambae wafanyakazi wenzako na marafiki kule mitaa ya stool ndefu na kwingineko wanakuona
 
dunia imejaa mengi ya kujifunza wajemeni, mweeeeeeh! umeufanya usiku na wikendi hii iwe ya tafakuri kubwa maishani mwangu. ubarikiwe saana
 
Na huu ni mwisho wa mwezi,nmifuko imekaa vyema kwa waajiriwa,hivyo kama unaijali familia itoe out kidogo wakabadilishe mazingira.
 
Wakati unapoamua kuwaona marafiki na watu wengine nje kuwa ni wa muhimu zaidi ya familia yako ni muhimu pia ukajiuliza swali hili...

KAMA LEO NAFUKUZWA KAZI NA SINA TENA HELA ZA ROUND WALA SIFA MTAANI, NITAKIMBILIA WAPI? Bila shaka ni kwenye familia yako

Invest all your resources and efforts kwenye familia kwani unauhakika it will be there for you .............
 
dunia imejaa mengi ya kujifunza wajemeni, mweeeeeeh! umeufanya usiku na wikendi hii iwe ya tafakuri kubwa maishani mwangu. ubarikiwe saana

Kikomo cha kujifunza ni kuamua kutokujifunza na sio kwa sababu hakuna vipya vya kujifunza..........Ubarikiwe sana kaka, si unajua mtu wa kwanza anekufahamu wewe zaidi ni mwenza wako zaidi? Huwa kila wafanyakazi wangu wanaposema jambo la kunisifia huwa najiuliza "JE NIKIMSIMAMISHA MKE WANGU ATASEMA HAYA KWELI, AU ATASEMA KINYUME"

Na huu ni mwisho wa mwezi,nmifuko imekaa vyema kwa waajiriwa,hivyo kama unaijali familia itoe out kidogo wakabadilishe mazingira.

Hahahaaaa, mkuu umenifanya nimecheka sana...........ipe raha familia yako bana, ni fahari ya pekee, watu wanatamani kuwa nayo lakini ndio hivyo wengine hawaweza kutokana na sababu kadha wa kadha
 
Umesema keli kabisa, Tatizo linakuja pale mtu ana nyumba ndogo tatu.
 
Marafiki wana umuhimu wao...familia nayo ina umuhimu wake.Hujawahi kuona watu wanakimbiwa na familia/ndugu zao mambo yakiwaendea kombo??Wape wote nafasi zao ili siku ukiwahitaji wale watakaokua tayari kusimama na wewe wafanye hivyo badala ya kuwatenga sasa hivi bila kujua yupi anaekujali kweli.
 
Umesema keli kabisa, Tatizo linakuja pale mtu ana nyumba ndogo tatu.

Hahaaaa, sasa hili mkuu linahitaji mjadala mwingine.........but all in all, tunza familia yako, hata kama unazo kumi, let them feel and enjoy kwamba wewe ni baba yao.....sio sifa za kwenye stool ndefu halafu ukifika home lol!!!!
 
dunia imejaa mengi ya kujifunza wajemeni, mweeeeeeh! umeufanya usiku na wikendi hii iwe ya tafakuri kubwa maishani mwangu. ubarikiwe saana

umeonae,yaani hii inamgusa kila mwenye family,whaaaoo!newD
 
Nakubali Lizzy, wana nafasi yao japo hii ni topic nyingine

Hapa nazungumzi wale ambao kwa marafiki 100% lakini wakirudi nyumbani watoto na mama wana hali ngumu........hope you get my point
 
Nakubali Lizzy, wana nafasi yao japo hii ni topic nyingine

Hapa nazungumzi wale ambao kwa marafiki 100% lakini wakirudi nyumbani watoto na mama wana hali ngumu........hope you get my point

Owwkeyyy
 
Nakubali Lizzy, wana nafasi yao japo hii ni topic nyingine

Hapa nazungumzi wale ambao kwa marafiki 100% lakini wakirudi nyumbani watoto na mama wana hali ngumu........hope you get my point

Wapenda maujiko. Kuna watu wanaweka heshima bar ilhali nyumbani kwake mlo wa shida, watoto kaptura zimetoboka toboka na wanapekua tu kama waziri wa bata huku mzazi anazungusha round za ukweli kwenye mabar mpaka anaitwa mheshimiwa.......SIO VIZURI!!!
 
Hahaaaaa, hii kali bana, mimi hapana sikia....wanapekua kama mawaziri wa bata lol.............HESHIMA NYUMBANI KWANZA BANA ndo safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…