Style Mpya ya Wizi wa Magari

Vocal Fremitus

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Posts
1,287
Reaction score
6,648
Wezi wa plate number za magari (Watekaji)
Kuna mtindo mpya wa utekaji umejitokeza. Watekaji wanakufuata pale unapo paki Gari lako hasa maeneo ya maegesho.

Unapo acha Gari lako kwenye maegesho watekaji au wezi wanaondoa namba za Gari lako yaani plate number, na wanakusubiria wewe urudi, ukirudi kuchukua Gari lako kwenye maegesho na ukaanza kuendesha kurudi uliko toka au kuelekea sehemu nyingine, wao watekaji hukufuata kwa nyuma, na huongeza mwendo na kukupita.

Huanza kukuonyesha Ile plate number ya Gari lako kwenye dirisha la Gari Yao, kama vile umeidodosha au umeipoteza wanataka kukurudishia kama watu wema waliyoiokota, wanataka kukurudishia.

Utakaposimama ili kuchukua Ile plate number ya Gari yako, wanakutolea bunduki, unatoka nje wanachukua Gari lako, na wewe wanakuteka pia na kukuchukua.

Mpango mahususi uliopangwa vizuri na hao majambazi, na kitendo kinachofanyika kwa haraka na kwa muda mfupi sana. Hata wenye magari wengine sio rahisi kugundua unachotendewa au kujua utekaji huo, maana wataona ni kama umesimamisha Gari lako wewe mwenyewe.

Tafadhali wajulishe na wengine hatari hii waijue. Usikae na Habari hii sambaza na wengine wapate uelewa [emoji1317]

C&P
 
Huu utekaji unafanyika hapa Tanzania au kwenye movie?
 
That why namiliki gari bovu, hakuna mwenye uwezo wa kuliwasha zaidi yangu Mimi[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Inasikitisha unajichanga unanunua gari kali alafu bado linakukosesha amani ya moyo na usingizi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umetisha mkuu.
 
japo si nzuri ila nimeipenda wezi wameanza kuiba kwa akili sio kibwege bwege
 
hizi hizi IST zinaibwa au kuna nyingine....gari zenyewe bongo chakavu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ