SUA ni Chuo au kituo cha ufisadi?


Bazazi ni JINA. Hebu soma post za juu, kuna member anajiita BAZAZI.
 

Samahani Mpita Njia. Hayo ndo matatizo ya majina yetu JF. Kama umesoma postings zote utagundua kuna mtu anaitwa Bazazi. Ndo maana niliandika Bazazi na siyo bazazi kama wewe ulivyoandika.

Najaribu kuweka maoni yake. ya Warsha. Na ndo maana unachanganya kwamba labda ni ya kwako.
 
JF musishangae,
Ni kama nilivyokuwa nimeeleza matatizo ya SUA.

Kuna hiyo Thread inayotufahamisha masharti mapya ya kurudishwa kwa wanafunzi UDSM, likiwemo la kufutwa kwa DARUSO.

Sasa taarifa niliyopewa ni kwamba kumbe SUA ilifuta siku nyingi chama cha wanafunzi kiitwacho SUASO. Ina maana kwamba hadi mgomo huu uliopita SUA hapakuwa na uongozi wa wanafunzi.

Unaijua sababu?
Ni kwamba uongozi mpya ulipoingia, ulitaka kujiepusha na migomo. Ukalipia kampeni za uchaguzi kwa mtu waliyemtaka awe puppet wao. Kama kawaida wanafunzi hawakusikia hilo. Akachaguliwa kipenzi cha wanafunzi. Kwa kuchukizwa na hilo, uongozi ukampa pesa aliyeshindwa aend mahakamani kuweka pingamizi.

Baadaye uongozi hautambui serikali ya wanafunzi.

sasa hebu tunaofahamu maisha ya Vyuo vikuu, ni wapi utaongoza wanafunzi bil aviongozi??

Hicho Chuo tusema kina VC na wasaidizi walio makini kweli?
Hicho Chuo kinaweza kupanga mambo ya maana kweli?
Hapo kuna mfano wowote unaoweza kuwa ni wa kuigwa na wanafunzi?

rubbish!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…