Chris Lukosi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 4,583
- 2,944
Ndugu zanguni,
Siku hizi kila mwanasiasa akipanda jukwaani anatumia kauli mbiu ya ukosefu wa ajira kwa sababu tayari limekuwa tishio kwa taifa. Wanasiasa hao kutoka pande zote, upinzani na tawala wote wanalia na suala la ajira kwa sababu ni suala linalomgusa kila mwananchi.
Mimi binafsi linanikera na kuniogopesha kwani ikifikia mwaka 2020 ina maana kama hatuja act sasa basi tutakuwa na wapiga debe wenye degree na waendesha boda boda wenye Phd.
Lakini kabla hatujakwenda mbele, ningependa tu kuwajuza kuwa suala la ukosefu wa ajira sio tatizo la Tanzania pekee, bali ni la dunia nzima na hii inatokana na ongezeko la watu duniani.
Kwa maoni yangu, napendekeza serikali ifanye yafuatayo kuongeza ajira nchini
1. Serikali ijenge au iite wawekezaji kujenga viwanda vya kudhalisha vitu ambavyo ni vya mahitaji ya lazima kwa binadamu nchini, kama vile nguo, bidhaa za plastiki, vifaa vya ujenzi, zana za kilimo, viatu nk. Kwa kufanya hivyo wataongeza nguvu kwenye kilimo kuzalisha malighafi na ajira kwa wale watakaohusika kuanzia kwenye uzalishaji mpaka uuzaji wa hizo bidhaa. Sio kila kitu lazima tutegemee china, mengine tunaweza kuyafanya nyumbani bila hata kuuliza.
2. Wakandarasi wa nje wakipewa kazi lazima waajiri aslilimia 99 % wazawa (mkandarasi asiruhusiwe kuleta madereva wa vidampa kutoka China)
3. Serikali irudishe miradi ya mikoa kama vile makampuni ya uchukuzi, maduka ya RTC, NMC nk.
4. Serikali iweke kitengo cha kufundisha ufundi kwenye kila sekondari kata ili kuwawezesha wale ambao wangependa kuja kuwa mafundi waweze kusomea fani wazipendazo badala ya kumlazimisha mtu kusoma sayansi kimu wakati unajua haina ajira hata akipata Phd.
5. Tanroads ichukue jukumu la kutunza na kukarabati barabara zote nchini na kuajiri wasomi na wasio wasomi kwa ajili ya hizo kazi, hii itapunguza ajali na kuboresha barabara zetu badala ya kuwapa wakandarasi wachovu kutunza barabara (mashimo yatakwisha mjini) Wakandarasi wapewe kazi za ujenzi wa barabara tu, kutunza na kukarabati iwe chini ya serikali
6. Serikali iongeze ukubwa wa jeshi la polisi kwa kuwaajili polisi jamii (mgambo) na kuwapa majukumu ambayo wanaweza kuisaidia polisi kama vile kukamata vibaka, kulinda mabenki, kulinda mikutano, kufanya doria za usiku na mchana jambo ambalo si tu litajenga ajira bali litapunguza uharifu.
Hayo ni mawazo yangu binafsi tu, lakini najua wengi wana michango yao ambayo serikali ikichuja pumba na mchele watapata walao moja la kusaidia