Mjomba/Shangazi suala hapa si wasomi wala wanasheria, kinachotakiwa ni wananchi wenyewe kuamua kuwa sasa basi. Wanachotakiwa ni kuwatoa viongozi hawa ambao hawana huruma na wanachi wanao watawala. Wao shida za wanaowatawala waziwapi taabu hata chembe, wanachofanya ni kuwaibia wananchi kwa mikataba mibovu kama hii ya dowans, mpaka wanananchi wanaoibiwa watakapo amua wao wenyewe kuwang'oa hawa mafisadi ndipo watakapo pona na kulipa hayo mabilioni ya dowans. Hata libya kwa sasa NTC hawahangaiki na kulipa mikataba kama hii ya dowans iliyo achwa na khadaffi.