Suala la kuajiri kwa kutaka mtu awe kapitia JKT liangaliwe upya, JKT huwa hawachukui wote wanaomaliza kidato cha sita mafunzoni

What a paranoid soul! Ni kitu kinachojulikana, ninakushangaa haukujua muda wote huo. 😀
 
Sijakuelewa...nachojua Mimi jkt huwa wanatangaza second selection baada ya wiki3 wakiona namba haijatimia....halafu watu kibao Tu sio hata TISS huwa wanajipeleka...Mimi mwenyewe kambi nliloenda sikuchaguliwa huko nlichaguliwa kwingine lakini Wala hata sikuulizwa ,nilipofika wakatuandika majina Tu tukaanza mzigo...walkuja kuanza kufatilia majina ya Ambao hawakuchaguliwa Hilo kambi kipindi cha ugawaji wa posho mwisho wa mwezi Na wote tuliozamia tukaandikwa majina ili posho yetu iletwe Basi. Wala hawakuwahi kutuuliza kwanini tumekuja apo
 
Hivi,kuna watu walikaa mahali na kuja na hayo maelekezo kwenye tangazo au limetengenezwa sehemu fulani tu?
Kwamba watengeneza tangazo hawana ndugu ama watoto wao watakaoathirika kwa mtindo huu?
 
Mawazo ya kitumwa tumwa haya,
Wakenya huwa wanasema kuandikwa kazi
Wewe beba mikanda miwili, soksi jozi mbili,
Mifuko miwili, vikombe viwili hata vya plastiki, sahani mbili simama barabarani tayari unapiga pesa
 
In fact ni ubaguzi. Kuna wengine kwa sababu za hali zao kiafya na kimaumbile (wenye ulemavu kwa mfano) hawawezi kwenda JKT, ina maana hawatapata ajira hizo husika?
JKT ya mujibu wa sheria haijalishi una ulemavu wa viungo wote Wana hudhuria kozi,
 
Kwani ajira zotee zinahitaji mtu awe amepita jkt? Kwa ambae hajapita jkt ataomba sehemu ambazo hazihitaji sifa za kupita jkt.Over! Ajira zipi zinahitaji mtu awe kapita jkt?
JWTZ kwa recruit ambao hawana diploma kupanda juu huwa lazima awe amepita JKT na Hawa wa diploma, degree, masters nk huwa ni special intake ndio maana hawaweki ulazima wa kipengele Cha kupita JKT
 
Ni vigezo vimewekwa, tuna weza kubaliana hata ambaye hana cheti nae ashindane na wenye vyeti... Taifa letu sote hivyo kujenga au kubomoa ni juu yetu
 
Kwani ajira zotee zinahitaji mtu awe amepita jkt? Kwa ambae hajapita jkt ataomba sehemu ambazo hazihitaji sifa za kupita jkt.Over! Ajira zipi zinahitaji mtu awe kapita jkt?
Kama vile magereza,police,na uhamiaji sifa mojawapo uwe umepitia jkt na aliyemaliza mgambo yeye hapana wakati wote wanafundishwa na jesh la wananchi hii imekaaje Ina maana washauri wa mgambo mkoa na wilaya msisumbue vijana kucheza mgambo maana mmeshindwa hata kuwatetea serikali kupata ajira shame in you
 
Ni vigezo vimewekwa, tuna weza kubaliana hata ambaye hana cheti nae ashindane na wenye vyeti... Taifa letu sote hivyo kujenga au kubomoa ni juu yetu
Kikubwa inputs za mtu na ubunifu in problem solving tu basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…