Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 308
Kwa mara nyingine tena tunashuhudia jinsi serikali yetu isivyo na vipaumbele, suala la katiba ni suala la haraka lakini siyo kwa namna ya dharura ya serikali.
Muswada ambao tunatakiwa tuujadili tarehe 7 & 8 April ndio utatufikisha kwenye katiba mpya ajabu ni kwamba ni Dodoma na Dar es Salaam tu ndio wamepewa fursa ya kutoa maoni yao, na kibaya zaidi kwa kipindi kifupi sana (leo kuna taarifa kuwa Dodoma kuna vurugu kwa sababu watu ni wengi kuliko ukumbi uliotengwa).
Kwa nini maeneo mengine hayajasikilizwa? Kila eneo lina changamoto za aina yake na kwa muswada wenye uzito wa aina hii ulipaswa usiwe wa dharura kiasi hiki na wadau wote angalau wapate muda wa angalau mwezi mmoja kuujadili na kutoa mapendekezo yao, siyo siku moja.. ina maana watanzania wanaoishi Kigoma, Musoma, Lindi, Wete, Namanga, kwa mfano hawana haki ya kusikilizwa. Au watanzania wanaoishi vijijini (zaidi ya 80% ya watanzania) hawana umuhimu kwenye huu mchakato wa katiba?
Napendekeza wabunge wakatae dharura ya aina hii ili wadau wapewe angalau mwezi mmoja kuchangia mawazo yao.....