Suala la maandamano tuwaachie wakenya pekee, maandamano ya Uganda yameshatulizwa, Maandamano Tanzania hatuna muda nayo

Hata Omar Al Bashir alisema hivi hivi mwaka 2019. Huyu bado nchi za Western hazijamchoka vizuri, ikifika point ya kumchoka vizuri muda utaamua.
Al Bashir ni wanajeshi wanaopigana Leo ndiyo walichochea maandamano,wakageukana baada ya Bashir kuondoka,Uganda watoto tu baleghe zinawasumbua wanaandamana
 
Tanzania na Uganda ni rahisi kutisha sababu wananchi ni waoga, hii hupelekea hata maandamano kuwa na watu wachache inakuwa rahisi mno kuyamaliza.

Achana kabisa na kitu kinaitwa nguvu ya Umma,
Wananchi wa hizo nchi wanajua Dola huwashukia vipi wakikaidi amri, Kenya polisi wanapiga selfie na waandamanaji!!
 
Al Bashir ni wanajeshi wanaopigana Leo ndiyo walichochea maandamano,wakageukana baada ya Bashir kuondoka

Unadhani kwanini jeshi ambalo limemtii kiongozi kwa miaka zaidi ya 30 linaamua kuchochea maandamano na kumgeuka amiri jeshi?

Hivi vitu havitokei kwa bahati mbaya, viko planned. Thats why nimesema bado nchi za western hazijamchoka vizuri, muda wa kufa nyani ukifika hata wale uliokuwa unawaamini, wakikutii na kukupigia salute wanakugeuka tu.
 
Al Bashir alipopindua alikua kibaraka wa nani?.. siasa za Sudan zipo kivyake,wakuu wa nchi ni wanajeshi kwenye vazi la kiraia,haya hizo pande zinazopingana ni vibaraka wa nani!?
 
sISI NI MAITI, MAITI HAZIFUFUKI ZIKAFANYA LOLOTE
 
Ujasiri wa vijana wa Kenya wa kuwa tayari kufa kutetea haki, wameionesha dunia kwamba vijana ni Taifa la LEO sio KESHO. Wapewe maua yao vijana wa KENYA!😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…