Suala la maoni ya katiba mpya

Suala la maoni ya katiba mpya

keulankubha

Member
Joined
May 7, 2012
Posts
49
Reaction score
13
Watanzania suala la kutunga katiba mpya ni jambo la msingi sana.
Jambo la kwanza la kuangalia majukumu ya Rais kwa ujumla katika katiba hii iliyopo ni makubwa sana. Mfano wa kuteua wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na mawaziri. Sioni kuwepo kwa wakuu wa mikoa na wilaya. Kwa mtazamo wangu sehemu moja iondolewe haina maana yoyote katika nchi changa kama hii Tanzania. Mtu wa kuondolewa ni mkuu wa wilaya tubaki na wakurugenzi wa wilaya na wakuu wa mikoa. i) Pia wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi katika mikoa yao, ili uwepo ushindani wa kuinua uchumi wa maendeleo ya mikoa, wilaya na taifa kwaujumla. Ili swala liingizwe kwenye katiba mpya. Viongozi hawa wakichaguliwa na wananchi watasimamia na kuimalisha uchumi na maendeleo ya mikoa, wilaya na kitaifa tena kwa ushindani mkubwa kwa masilai ya wananchi
ii) Wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe wagombea wa chama chochote cha siasa katika katiba mpya. Rais tunaye mtaka Katika katiba tunayoitaka wananchi tutoe maoni yetu juu ya rais tunayemtaka i) Rais awetayari kuwajibika na kufikishwa mahakamani itakapo bidi. Pia ikumbukwe kuwa katiba yetu haina chama chochote kiwe chama tawala au chama chochote cha siasa. ii) Katiba ioneshe wazi kuwa mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mgombea urais awe amekubaliana na masharti ya katiba hii. Kuwa yuko tayari kuwajibika/kuwajibishwa na kufikishwa mahakamani pale itakapo bidi. Huyo ndiye rais tunayemtaka, sio kwamba tumsikilize yeye anayoyataka. Katiba hii mpya iweke wazi. iii) Pia katiba mpya ioneshe wazi kuwa rais anao wajibu wa kuteua mawaziri kwa kuzingatia yafuatayo:- a) Kwanza mawaziri/waziri atakaye teuliwa na rais awe chini ya uangalizi kati ya miezi sita (6) au muda usio zidi mwaka mmoja (1). b) Baada ya miezi sita (6) au mwaka mmoja itakavyokuwa imepitishwa kabla ya kuapishwa kuwa waziri kamili, yawepo maoni ya wananchi kumkubali au kumkataa kulingana na utendaji wake wa kazi wa miezi sita (6) au mwaka mmoja aliokuwa katika uangalizi. Speaker wa bunge Katiba mpya ipunguze mamlaka makubwa aliyonayo speaker wa bunge, kwa masilai ya wananchi na taifa kwa ujumla. mfano katiba iliyopo imempa mamlaka makubwa kuamua yeye atakavyo kulingana na mamlaka aliyonayo. Speaker wa bunge apewe mamlaka lakini yawe na mpaka. Pia maamuzi ya bunge yawe ndio ya mwisho maana bunge ni chombo kikuu kwa niaba ya wananchi kusimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mjibu wa katiba.
 
Remember that "God will not give any solder ammunition who does not willing to go into battle"
 
Mawazo yako ni safi. Sasa ili yatekelezwe, peleka mapendekezo yako Tume ya Katiba ili yajumuishwe na mengine. Fanya hima, muda unayoyoma!
 
Back
Top Bottom