Suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kufundishia laibuka tena Bungeni

Suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kufundishia laibuka tena Bungeni

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Suala la matumizi ya lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia laibuka tena Bungeni wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Elimu leo tarehe 7/04/2024.

Akichangia hoja Mbunge kutoka zanzibar ndg.Shamsi vuai imeishauri Wizara ya Elimu kutumia Lugha ya Kiswahili katika kufundisha masomo mengine pia ameshauri Lugha ya Kiingereza ifundishwe kama lugha na pia kuwe na wataalamu wa lugha hiyo walio bobea.

Kinacho nishangaza mimi binafsi ni; nani haswa anaye zuia lugha ya kiswahili kutumika??! nani alaumiwe?! Kama sisi sote ni watanzania wa kuzaliwa kwanini tunakuwa na kigugumizi ktk kuamua juu ya matumizi ya lugha yetu ya kiswahili?

Viongozi wetu lazime wawe na utashi wa kuamua ili huu mjadala ufikie mwisho, kila mwaka jambo hili linaibuka!
 
Suala la matumizi ya lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia laibuka tena Bungeni wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Elimu leo tarehe 7/04/2024.

Akichangia hoja Mbunge kutoka zanzibar ndg.Shamsi vuai imeishauri Wizara ya Elimu kutumia Lugha ya Kiswahili katika kufundisha masomo mengine pia ameshauri Lugha ya Kiingereza ifundishwe kama lugha na pia kuwe na wataalamu wa lugha hiyo walio bobea.

Kinacho nishangaza mimi binafsi ni; nani haswa anaye zuia lugha ya kiswahili kutumika??! nani alaumiwe?! Kama sisi sote ni watanzania wa kuzaliwa kwanini tunakuwa na kigugumizi ktk kuamua juu ya matumizi ya lugha yetu ya kiswahili???!!!

Viongozi wetu lazime wawe na utashi wa kuamua ili huu mjadala ufikie mwisho, kila mwaka jambo hili linaibuka!!!
Waanze kwa kuwatoa watoto wao kwenye shule zinzotumia lugha ya kiingereza kufundishia.
 
Huhitahiji kuforce lugha, lugha ni wimbi, unategemea limekuja na nini? Elimu ya maarifa na ujuzi kwetu ni adimu waljojitolea kuachia ije kwetu hawana Kiswahili, Sisi ndio tumewapokea na lugha yao, Utamaduni wa ulaya ni wimbi lililokuja na Civilization Mpya ndio maana ikiingia Tanzania Kwa Mara ya Kwanza unaweza ukaona umepinga nchi ya lugha ya Kiingereza Kwa mawasiliano, mfano Mabango ya Barabarani, taasisi za wananchi na Serikali, mengi Ni ya Kiingereza, magari ya jeshi, English tupu.
Na Maisha yanaenda. Tuache kuongeza gharama Kwa kurudi Nyuma, twende tu na rolling ya Utamaduni. Utamaduni ni huru na hauna mipaka Ila unaenziwa tu.
 
Mada nzuri Kama hizi huwa zinakosa wachangiaji sijui kwa Nini!! Watu hawafahamu kwamba kelele zote humu Tanzania za umasikini 95asilimia inachangiwa na swala hili la kingereza Kama somo la kufundishia.

Siri ambayo wasomi wengi wameshindwa kuigundua na kubaki na jazba pindi unapogusia kwamba kiswahili kitumike Kama lugha ya kujifunzia msingi Hadi elimu ya juu.

Tutakamatana uchawi sana, tutatekana, tutalia na ufisadi Sana tu, tutalia na umasikini wa kipato na fikra sababu kubwa ikiwa Ni hii hii "kiswahili Kama lugha yakufundishia kwa awali Hadi elimu ya juu"

Wasomi wamelewa na mvinyo wa kupenda kutukuzwa na kusifiwa kisa tu eti wanaongea kingereza nakushindwa kujua kwamba kingereza Ni lugha Kama lugha nyingine

Viongozi wa nchi wangetambua kwamba lugha hii ya kiingereza inasababisha vifo vingi kwa wananchi , sidhani Kama wangeweza kuruhusu lugha hii kutumiwa mashuleni. Inavunja moyo kwakweli. Maana Jambo la msingi Kama hili halipewi kipaumbele. Niko pale nimekaa.
 
Back
Top Bottom