Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Akiongea mbele ya waandishi wa habari, alisema kuwa ana uthibitisho kuwa hata mmiliki wa stationery, alipewa kibali Cha kuagiza Sukari nje ya nchi!
Hata hivyo kitu Cha ajabu sana ni hiki kilichotokea Bungeni Jana, Kwa Spika wa Bunge, Tulia Ackson kuamuru Mbunge huyo, Luhaga Mpina, aburuzwe Kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, eti Kwa kumdharau yeye Spika wa Bunge, Kwa kutomletea yeye ushahidi huo na badala yake kuupeleka Kwenye vyombo vya habari!
Tunafahamu kuwa vyombo vya habari ni mhimili wa 4 wa Dola, ambao unapaswa kufichua uovu wote unaofanyika hapa nchini.
Wananchi wote wa nchi hii, tunapaswa kusimama na Mbunge Luhaga. Mpina, Kwa kuwa inaonekana dhahori kuwa huyu Spika Tulia Ackson, anataka kuligeuza Bunge letu, kuws ni sehemu ya kuwalinda wale wanaovunja sheria za nchi hii.
Hivi kosa la Mbunge Luhaga Mpina, ni lipi hasa, hadi aburuzwe Kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge??
Hili Bunge letu, limezidi kuthibitisha udhaifu wake, ambao sisi wananchi tumekuwa tunauona Kwa kipindi kirefu sasa.
Pia soma:
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili
- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
- Wananchi tunamsaidiaje Mpina?
- FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi Wa Luhaga Mpina Kwa Spika Wa Bunge Dkt Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe Kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari