Suala la Mipango miji bado ni changamoto Tanzania

Suala la Mipango miji bado ni changamoto Tanzania

Sappire

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2024
Posts
3,447
Reaction score
8,896
Hivi wenzetu wafaransa waliweza vipi kupangilia vizuri namna hii miji yao.mfumo wao wa ujengaji makazi ukoje ?

Ukilinganisha na hapa kwetu Dar ambapo ndiyo wtz wengi wanapasifu,unaona kabisa utofauti mkubwa.Nini kifanyike ili na sisi miji yetu ipendeze?

Mimi napendekeza wanaohusika na mipango miji wakajifunze Kwa wenzetu ili wapate uzoefu.Na wewe pendekeza ambacho unaona kinafaa kufanyika ili miji yetu ipendeze kama ya wenzetu.

Picha Moja ni jiji la Paris na nyingine ni jiji la Dar es Salaam

Screenshot_20240811-174515.jpg

Screenshot_20240811-180047.jpg
 
Tanzania kuna shida kubwa sana Halamshauri zetu zina watu mbumbumbu hawajawahi kutoka nje mtu kasoma Mbeya akafanya Master Mzumbe unampeleka kuwa DED Ilala unadhani atakaa afanye nini
 
Hivi wenzetu wafaransa waliweza vipi kupangilia vizuri namna hii miji yao.mfumo wao wa ujengaji makazi ukoje ?

Ukilinganisha na hapa kwetu Dar ambapo ndiyo wtz wengi wanapasifu,unaona kabisa utofauti mkubwa.Nini kifanyike ili na sisi miji yetu ipendeze?

Mimi napendekeza wanaohusika na mipango miji wakajifunze Kwa wenzetu ili wapate uzoefu.Na wewe pendekeza ambacho unaona kinafaa kufanyika ili miji yetu ipendeze kama ya wenzetu.

Picha Moja ni jiji la Paris na nyingine ni jiji la Dar es Salaam

View attachment 3067032

View attachment 3067052

Sasa sisi si Waafrika hata tukiwekewa kanuni tunazivunja tu, na hata hao walioweka kanuni walifanya hivyo ili waingie tu kwenye kikao cha posho...
 
Tatizo hiyo Taaluma ya Mipango Miji ilianzia huko kwanza,halafu tukajaletewa sisi wakati tayari tushaharibikiwa.
 
Issue siyo watu waende huko Ulaya,America au Japan.Issue zinaanzia hapa:
1.Miji ni kitu kigeni Kwa Mwafrika,alikuwa akikaa porini,na wanyamapori na Mifugo (Mingine analala nayo ndani-Mbuzi na Kuku wengi tumelala nayo,labda wachache).Ukiwa Kijijini unaelewa vizuri hii kitu.
2.Wakoloni wanapokuka wakatukuta hivyo kienyeji.Walianza kuupanga Mji wa Mzizima,ukirejea Masta plan ya Dar.Kule Kivukoni Hadi Oyster bay walikaa wazungu,Upanga wahindi na Kariakoo wabongo.Tunapopata Uhuru tukaanza kurejea Maisha yetu ya bila utaratibu,bila kufuata Sheria.

3.Hapa Afrika ni Nchi chache Sana ziko na mpangilio wa Miji-Ukiwa unashuka Pretoria au Durban au Johannesburg au Nairobi,au Cairo na Zamani Harare unaweza kuona mpangilio mzuri.
Standard ya Mpangilio huanza na Miundombinu Kwanza ya Barabara,reli,Maji Safi na majitaka,Huduma za Jamii kama Elimu,Afya na Masoko kisha watu Kupewa Viwanja. Ukifeli hapo watu wanaanza Kujenga kabla ya miundombinu Itakuwa ngumu Sana kutatua.
4.Kwa mbali Sana angalau Dodoma kuna Mitaa Kadhaa imepangiliwa hasa Ile ya Zamani,na Miji michache kidogo kama Makambako na Nzega.Kwingineko ni style Ile ya wanakijiji wanaingia Mjini,Wanajenga popote bila Kibali,kisha wanaanza kukumbuka Barabara huku wako ndani.
Pa kuanzia ni Serikali Kupima Maeneo Kwanza kama walivyojaribu Tunasoma au Bunju,kuweka miundombinu kisha Kuuza Viwanja.
Ukitaka Dar iwe na Mpangilio Omba tetemeko livunje Nyumba zote kisha Tuanze upya.
 
Factors zilezile
Poor capital
Poor infrastructures
Poor technology
Hivi ndivyo mmekaririshwa. Hakuna factor hata moja hapo.

Factor ni moja tu, Poor Mental Capacity. That's it. Kama ukikosa critical thinking hata upewe billion 10 za kimarekani, hautofanya chochote. Na bila ya critical thinking kamwe hauwezi tengeneza intricate infrastructures na sahau kabisa kuhusu advanced technology.

Wewe mkuu ni evidence tosha ya nilichokiandika.
 
Na Ndio Maana waliwatandika mijeledi wazee wetu
Sio kwasababu walikosa akili. Bali kwa sababu hawakujiandaa na hawakuwahi kupambana wala kukutana na advanced civilization yenye silaha kali na waliojipanga kuwa-exploit kilazima. Ni kama leo washuke watu wa ajabu wenye rangi ya kijani wakiwa na silaha kali za ajabu na wamejipanga kukugeuza ng'ombe wao.
 
Hivi wenzetu wafaransa waliweza vipi kupangilia vizuri namna hii miji yao.mfumo wao wa ujengaji makazi ukoje ?

Ukilinganisha na hapa kwetu Dar ambapo ndiyo wtz wengi wanapasifu,unaona kabisa utofauti mkubwa.Nini kifanyike ili na sisi miji yetu ipendeze?

Mimi napendekeza wanaohusika na mipango miji wakajifunze Kwa wenzetu ili wapate uzoefu.Na wewe pendekeza ambacho unaona kinafaa kufanyika ili miji yetu ipendeze kama ya wenzetu.

Picha Moja ni jiji la Paris na nyingine ni jiji la Dar es Salaam

View attachment 3067032

View attachment 3067052
Waliwekeza kwenye taaluma badala ya siasa
 
Back
Top Bottom