Issue siyo watu waende huko Ulaya,America au Japan.Issue zinaanzia hapa:
1.Miji ni kitu kigeni Kwa Mwafrika,alikuwa akikaa porini,na wanyamapori na Mifugo (Mingine analala nayo ndani-Mbuzi na Kuku wengi tumelala nayo,labda wachache).Ukiwa Kijijini unaelewa vizuri hii kitu.
2.Wakoloni wanapokuka wakatukuta hivyo kienyeji.Walianza kuupanga Mji wa Mzizima,ukirejea Masta plan ya Dar.Kule Kivukoni Hadi Oyster bay walikaa wazungu,Upanga wahindi na Kariakoo wabongo.Tunapopata Uhuru tukaanza kurejea Maisha yetu ya bila utaratibu,bila kufuata Sheria.
3.Hapa Afrika ni Nchi chache Sana ziko na mpangilio wa Miji-Ukiwa unashuka Pretoria au Durban au Johannesburg au Nairobi,au Cairo na Zamani Harare unaweza kuona mpangilio mzuri.
Standard ya Mpangilio huanza na Miundombinu Kwanza ya Barabara,reli,Maji Safi na majitaka,Huduma za Jamii kama Elimu,Afya na Masoko kisha watu Kupewa Viwanja. Ukifeli hapo watu wanaanza Kujenga kabla ya miundombinu Itakuwa ngumu Sana kutatua.
4.Kwa mbali Sana angalau Dodoma kuna Mitaa Kadhaa imepangiliwa hasa Ile ya Zamani,na Miji michache kidogo kama Makambako na Nzega.Kwingineko ni style Ile ya wanakijiji wanaingia Mjini,Wanajenga popote bila Kibali,kisha wanaanza kukumbuka Barabara huku wako ndani.
Pa kuanzia ni Serikali Kupima Maeneo Kwanza kama walivyojaribu Tunasoma au Bunju,kuweka miundombinu kisha Kuuza Viwanja.
Ukitaka Dar iwe na Mpangilio Omba tetemeko livunje Nyumba zote kisha Tuanze upya.