Luhungu
JF-Expert Member
- Sep 5, 2013
- 817
- 237
Shule zimefunguliwa takribani siku Nne Hadi Sasa na kwa uhakika wanafunzi wa Kidato Cha kwanza Wana miminika mashuleni.
Uhakika uliopo ni kuwa wote wanakuja kuanza mtaala ulioboresha (alimaarufu mtaala mpay)
Pasipo kupinga mtaala ulioboreshwa umelenga kupunguza changamoto za mwanafunzi kuhitimu akiwa hana cha kuonyesha katika uhalisia huko mtaani katika maisha ya kawaida. Serikali naipongeza.
Changamoto yangu ni namna maandalizi yalivyo na namna uwazi na utekelezaji wake unavyo kwenda kuwa.
Ukitazama kwa umakini utangundua hata walimu watakao tekeleza mtaala huu, wengi wao ni Kama wanasubri nani afanye, maana hata wao hawaamini Kama ndo mtaala umeeanza.
1. Hakuna mafunzo stahiki
2. Ushirikishwaji ni mdogo na ama haupo kwa baadhi ya maeneo na
3. Utayari wa Walimu ni kama hawako tayari japo kwao tamko ni agizo.
Nashauri namna Bora na ya haraka ifanyike ikiwemo,
1. Uzalishaji/usambazaji wa vitabu na vitendea kazi stahiki
2. Semina wezeshi hasa katika kuliendea na utekelezaji wa jambo hili.
3. Vipindi elekezi vya radio, tv na namna nyingine ambayo itawapa Wazazi uelewa wa mapema dhidi ya kile Watoto wao wanacho kiendea.
Mwisho, Elimu ni Silaha, isitumiwe vibaya maana Taifa litaangamia.