Suala la Ndugai ni over-reaction, watawala jaribuni kuwa na ustahimilivu

Suala la Ndugai ni over-reaction, watawala jaribuni kuwa na ustahimilivu

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Naomba nitoe nasaha kwa watawala kujitahidi kuwa wastahimilivu kwa viongozi wenzao na wananchi wengine. Na pia wajitahidi kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazotoa nafasi pia kwa wangine bila kutumia mabavu.

Hili ni muhimu ukichukulia kwamba maisha ya binadamu hayategemei mamlaka pekee au ulinzi wa vyombo vya dola. Tukichukulia mfano wa mzee Mwinyi .aka. mzee Ruksa, siri yake ya kuishi miaka mingi huenda ni uwezo wake mkubwa wa kustahimili mapungufu ya wengine na changamoto mbalimbali na pia kuthibiti jazba.

Ni hayo tu kwa leo.​
 
Mtu anaongea kumchamba mwenzake anashika na kiuno kwa msisitizo.....tunaye
 
Sio tu over reaction ni Kuonyesha kwamba watu wengi hawajaiva kuwa Vongozi au hawana Vifua vya kuhimili challenges za Kiuongozi. Viongozi Viza katika madaraka.
 
Ustahimilivu na kuvumiliana ni vitu adimu sana katika uwanja wa siasa za Tanzania. Rejea fukuza fukuza ya wabunge wa upinzani toka bungeni iliyoongozwa na Anna Makinda na Ndugai, watu kupotezwa kisa wameikosoa siri-kali na wengine kupigwa risasi na kutiwa vilema vya maisha.
Chama changu kinafeli sana, kilitakiwa kiwe mfano wa kuigwa katika kuonesha political tolerance kwa watu wapinzani, Polepole, Gwajiboy na sasa Ndugai
 
Back
Top Bottom