James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Ngorongoro ni urithi adimu sama duniani mwenyezi mungu ametupa Watanzania. Tunatakiwa tuilinde kama mboni ya macho yetu.
Cha kusikitisha watu wanawatumia Wamasai kama kivuli cha kuhifadhi mifugo yao kwenye hifadhi ya taifa.
Watu wenye pesa wameifanya hifadhi ya Ngorongoro kama sehemu ya kuhifadhia mifugo yao. Watu hao wanawatumia Wamasai kwa kuwalipa fedha kidogo ili kuwachungia na kuwahifadhia mifugo yao. Inasemekana wanasiasa na askari wa wanyama pori pia ni kati ya watu wenye mifugo huko Ngorongoro.
Kama serikali ikiwaondoa Wamasai Ngorongoro watu hao pia wataathirika. Ndio maana wanajifanya "kuwatetea" Wamasai ilhali wanatetea matumbo yao. Pia wameanza kueneza propaganda eti serikali inataka kuwaondoa Wamasai ili kuwauzia eneo hilo mabeberu!