Suala la sukari liangaliwe kwa jicho pevu la kiuchumi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Kwa kipindi sasa raia wamekuwa wakilalamikia bei ya sukari kupaa na utetezi mbalimbali ukittoka kuhusu sababu ya kupaa kwa bei hiyo. Sababu ikitolewa kuwa ni mwezi wa ramadhani au kufungwa kwa viwanda. Vyovyote vile lakini imeshaonekana kuwa tunahitaji sukari kwa kipindi hiki na hivyo tunapaswa kuingiza sukari kutoka nje.

Serikali ilisema imeagiza tani 40,000 za sukari na ilishanza kupakuliwa, na ingeweza kuingia mitaani tangu Aprili 17 kwa ripoti za mamlaka zilizotolewa mwanzo. Nahisi kuna changamoto kwenye namna sukari hiyo inawafikia walaji, ndio sababu bado bei elekezi inalalamikiwa kutofuatwa maeneo mengi.

Nguvu ya soko ina maajabu yake, na ukitumia nguvu za kimamlaka kudhibiti nguvu ya soko, biashara haramu ‘black market; huwa ni matokeo. Kama baadhi ya watu waliolalama kuuziwa sukari na watu wanaowajua tu. Kuwakamata au kuwafutia leseni wafanyabiashara bado hakutashusha bei.

Ipo haja ya kuona kuwa kwa kipindi hiki tatizo la sukari lipo kwenye uzalishaji wake ‘Supply’, ambayo hii inaweza kuongezwa kwa kuruhusu sukari kutoka nje kwa kuangalia upya masharti ya uagizaji wa sukari. Upande wa uhitaji ni huwa unadhibitiwa zaidi na bei.

Hivyo basi ipo haja ya kuona sukari inaingia kwa wingi nchini na bei itashuka. Sukari isiingie kwa namba tu, bali iingie kwa uhakika, maana ni swala la kufikirika kuwa na tani 40,000 za sukari halafu bado sukari adimu.

Wala tusidhani kuwa kuna watu wanaficha sukari ndani mwao, na hata kama wanaficha sukari ikiwa nyingi hiyo wanayoificha itawadodea, kibiashara ufichaji wa bidhaa unaweza kufanyika iwapo bidhaa inaanza kuwa adimu, Bidhaa ikipatikana kwa wingi ni ngumu mtu kuihodhi.


Signed

OEDIPUS
 
Pamoja na kuagiza sukari na bidhaa nyingine, hasa kutoka China, Serikali iwe makini kama Kenya iilivyokuja kugundua (angalia video clip). Hii inanikumbusha uamuzi wa Rais Magufuli, kuhusu matokeo na vipimo vya COVID-19 ulikuwa sahihi
Your browser is not able to display this video.
 
Sukari kupanda lazima kuna wanufaika huko kwenye serekali ndo maana kila kukicha wanaichokonoa ili ipande.

Vip mafuta nilisikia yameshuka bei kwenye soko la dunia hapa kwetu vipi.
 
Kenya waligundua Nini?
Sent using LEAGOO M12
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…