Suala la ubaguzi wa rangi Marekani lina mzizi mkubwa

Suala la ubaguzi wa rangi Marekani lina mzizi mkubwa

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
1,598
Reaction score
1,822
Swala la ubaguzi wa rangi Marekani sio swala linalotokea kwa bahati mbaya. Chuki ya Mzungu dhidi ya mweusi sio tabia/hulka ya mtu. Ubaguzi Marekani unatokana na mfumo wa nchi hiyo, Wabaguzi wa rangi nchini Marekani hawajatokea kwa bahati mbaya bali mfumo ndo umetengeneza watu wa namna hiyo.

Mfano: Tazama video hapo chini, Namna watoto wa kizungu wakiwabagua watoto wakiAfrika huko nchini Marekani. Kwa nyuma utaona wazazi wao wakiwaangalia tu kama vile ni sinema ya aina fulani.

Hawa watoto ndio mapolisi, wanasheria, wauguzi wa sasa huko nchini Marekani.
 
Ubaguzi huwa upo tu. Cha msingi ni kila mmoja ajenge nahusiano yake binafsi na Mungu.

Kuna sehemu imeandikwa: "Mungu alimchukia Esau, akampenda Yakobo"
 
Ubaguzi huwa upo tu. Cha msingi ni kila mmoja ajenge nahusiano yake binafsi na Mungu.

Kuna sehemu imeandikwa: "Mungu alimchukia Esau, akampenda Yakobo"
Sidhani kama itasaidia maana wazungu wengi ni wapagani kwa sasa,
 
ubaguzi ni natural. Mzungu atambagua mweusi, mweusi atambagua (hata kumkata viungo) albino etc...

Cha muhimu kila mtu awe na self-respect basi, mengine yatafuatia
 
Acheni upumbavu wa kulalamika Kila mara, Kama unabaguliwa miaka yote hiyo karibia miaka 200 unafanya Nini Huko?
Mbona Kila siku mnapanda ma boat mnataka kuzamia Marekani na Ulaya?

Fanyeni kazi muendeleze kwenu na hakuna atakayewabagua
 
Hao wamarekani wamezaliwa huko huko, Na hawajui asili yao ni wapi haswa hapa Afrika
 
Hao wamarekani wamezaliwa huko huko, Na hawajui asili yao ni wapi haswa hapa Afrika
Mtu unaweza ukahama nchi hata Kama umezaliwa nchi nyingine, mbona Waafrika wengi wanahamia Marekani kwa maelfu kwa Nini wakati Kuna ubaguzi?
Iweje kuhamia Marekani iwezekane Ila kuhama isiwezekane?
 
Wengi hawana elimu mkuu, wanajua mnaishi kama bushmen hivyo wanaogopa kurudi.
 
Ubaguzi upo sababu watu weusi tuna inferiority complex mbele ya mtu mweupe ila hata sis wazungu tunawabagua ila haina madhara sababu wana superiority complex by nature mbele ya mweusi
 
Back
Top Bottom