#COVID19 Suala la ugonjwa wa Covid-19 Tanzania lazima liangaliwe kwa mapana

#COVID19 Suala la ugonjwa wa Covid-19 Tanzania lazima liangaliwe kwa mapana

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Ni wazi kuwa Tanzania tangu ugonjwa huu mkubwa ulipuke duniani kote tumeendelea kuchukua tahadhali ikiwa njia ya kutumia dawa zetu za kienyeji pamoja na kujifukiza hii njia ilituvusha mwaka 2020 na ndiyo maana hatukuweza kufungiwa majumbani na maisha yaliendelea kama kawaida.

Baada ya hayati Magufuli kuchukuliwa na Mungu serikali ya awamu ya sita iliunda kamati ya wataalam kuja na tafti ya ugonjwa huo ambapo mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema tanzania siyo kisiwa lazima tukubaliane na wenzetu kamati hiyo ilibaini kuwa ugonjwa huo upo Tanzania kutokana na taarifa iliyotolewa ikulu wakati wa makabidhiano wa nyaraka za taarifa za ugonjwa huo.

Ikumbukwe kwamba pamoja na nchi tajiri kufungia ndani watu wao na kupokea chanjo ya ugonjwa huo bado na kuwa na madaktari bingwa na vifaa tiba watu wao waliendelea kuangamia mfano mzuri india china n.k.

Sisi kama taifa tena taifa maskini kwanini tusiendelee kutumia mbinu iliyotuvusha mwaka 2020 tunaomba swala hili raisi alifikirie kwa kuwa hizo kamati alizoziunda zimepiga hela na hakuna tutakachofanikisha.

Tunakuomba mheshimiwa raisi tuendelee kutumia mbinu zetu tulizotumia.
 
Tumia wewe na familia yako hujalazimishwa, huyo aliyekuvusha bado yuko hai?
Kuna mtu alitumika kuvusha watu au ni kauli za chuki ambazo kamwe hazitoi mchango bali ni dalili za fikra duni.

Bandiko linajieleza vizuri kwa kuomba Serikali ya Awamu ya Sita isiingize Taifa kwenye mkumbo wa kuchukua hatua ambazo nchi nyingi, hata tajiri na majirani, zimechukua lakini bado gonjwa linatesa.
 
Tz hakuna hilo gonjwa la nanihii hilo. Msiongelee tena habari za kutisha watu. Acheni kabisa umbea.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mama na JPM si ni yule yule? Vipi tena hii kumbusha kumbusha ya gwiji wa UVIKO 19 huyu?

Zitakuwa dalili njema hizi?
 
Kwanza kabisa, thibitisha kamati zimepiga hela.

Ukishindwa hili, kubali wewe mzushi.
Endelea kuabudu wazungu
Screenshot_20210617-091708_Facebook.jpg
 
Kuna mtu alitumika kuvusha watu au ni kauli za chuki ambazo kamwe hazitoi mchango bali ni dalili za fikra duni.

Bandiko linajieleza vizuri kwa kuomba Serikali ya Awamu ya Sita isiingize Taifa kwenye mkumbo wa kuchukua hatua ambazo nchi nyingi, hata tajiri na majirani, zimechukua lakini bado gonjwa linatesa
Bana makalio ulale mkuu
 
Ni mbinu gani unazopendekeza zitumike, ambazo zimethibitishwa kutusaidia kama nchi?
 
Labda wewe Sexless useme ni mbinu gani ambazo Tanzania hatujatumia kupunguza maambukizi ya COVID-19 kiasi yako juu kuliko nchi nyingine?
Binafsi ninaamini huu ugonjwa haujatuathiri Sana watanzania kwasabbb fulani fulani. Yaweza kuwa ni za kijiografia, kibayolojia, kiuchumi ama kijamii ( Utafiti ufanyike kuzibaini).

Pasitokee mtu akajipa sifa ama akatoa sifa kwamba kuna mbinu imetumika kutupunguzia dhahama hii.

Tusidanganyane kwamba tupifanya maombi kuliko mataifa mengine?
Tusidanganyane kwamba ushirikina wetu wa kutumia nyungu umetuokoa.
Tusidanganyane kwamba kuna kiongozi fulani alimtumainia Mungu Sana akatuokoa.
 
Watoto wetu wanachomwa chanjo dhidi ya magonjwa ya kitoto kila uchao katika "clinics" zetu.

Ninajiandaa kuchomwa chanjo dhidi ya COVID-19 ikiwa serikali yetu adhimu ITATULETEA.

SIASA za "conspiracies" hazitusaidii.

Nitakuwa wa mwanzo KUKUBALI kuchomwa CHANJO hiyo.

#KaziIendelee
 
Binafsi ninaamini huu ugonjwa haujatuathiri Sana watanzania kwasabbb fulani fulani. Yaweza kuwa ni za kijiografia, kibayolojia, kiuchumi ama kijamii ( Utafiti ufanyike kuzibaini).

Pasitokee mtu akajipa sifa ama akatoa sifa kwamba kuna mbinu imetumika kutupunguzia dhahama hii.

Tusidanganyane kwamba tupifanya maombi kuliko mataifa mengine?
Tusidanganyane kwamba ushirikina wetu wa kutumia nyungu umetuokoa.
Tusidanganyane kwamba kuna kiongozi fulani alimtumainia Mungu Sana akatuokoa.
Umenena sahihi. Hoja yangu inapinga wanaotaka takwimu zitangazwe kwa kuwa imedhirika wazi kuwa kufanya hivyo huongeza hofu na woga.

Ujumbe uliomo kwenye kiambatanisho unajitosheleza kuhusu ugonjwa wa COVID-19 na njia sahihi za kujikinga dhidi ya maambukizi

IMG-20210617-WA0000.jpg
 
Suala tu la afya yako mpaka serikalini ikuambie nini unatakiwa kufanya jamani? Kama umeona kwamba njia zilizotumika mwanzo ni sahihi wewe na familia yako na watu wako wa karibu ni vizuri kuzifuata pia, suala la chanjo siyo la lazima na hayo ndo yalikuwa mapendekezo ya kamati
 
Back
Top Bottom