A
Anonymous
Guest
Imekuwa kawaida Mtumishi kusema ''nina mwaka 2,3 ,4 nk, nahangaikia swala la uhamisho na ugumu upo katika Ofisi za halmashauri hawataki kuruhusu mtu kuhama'', Mtu unaweza jaza kwenye mfumo (ess utumishi) shughuli inakuwa kwenye kupata authorization kutoka kwa wakuu wake, Na Wengine tayari walishapata vibari toka Tamisemi lakini Maafisa wa Halmashauri wanaficha barua/hawatoi ruhusa ya mtu husika kuondoka, inakuwa nenda rudi bila mafanikio.
Hali hii inatengeneza mianya ya rushwa na inapunguza hamasa yakufanya kazi kwa wale ambao bado hawaja kamilishiwa uhamisho wao, pia inamrudisha nyuma mtumishi katika mipango ya maendeleo yake Kikazi, kifamilia, kiuchumi nk.
Wenye mamlaka Tamisemi waangalie hili Watumishi tunapenda kazi lakini mazingira ya kiutawala ya halmashauri zetu yanakatisha tamaa. Unaweza fikiri hata kuacha kazi.